Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAANDISHI DAR WANUSURIKA KIFO KWA KIPIGO KAMA CHA MWANGOSI TOKA KWA ASKARI POLISI

isango

 

Isango 2Jeshi la Polisi katika kile kinachoelezwa kuwa ni kukosa mbinu za kuimarisha hali ya amani na usalama lilijikuta likitumia nguvu isiyo na lazima kukabiliana na mamia ya watu waliojitokeza kufuatilia sakata la kuitwa kwa mahojiano kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam jana.

Jambo baya zaidi ni kitendo cha Polisi kuwashambulia kwa kipigo kikali waandishi wa habari bila huruma wala kujali kujitambulisha kwao wakiwa kazini kukusanya taarifa za kuripoti kwa umma. Waandishi wengi waliumizwa na kupoteza vifaa vyao vya kazi kwa hali ambayo haikulazimu kufikia hapo.

Itakumbukwa pia Mwandishi Daudi Mwangosi na wengine kadhaa walipigwa tena na Polisi wakati wakifanya kazi yao huko Nyololo Mkoani Iringa na bahati mbaya Mwangosi akalipuliwa na bomu na kupoteza maisha hapohapo.

Pichani juu ni mwandishi Josephat Isango wa Tanzania Daima akikabiliana na kipigo kikali kutoka kwa Polisi watatu wenye silaha na yeye akiwa na kitabu chake na peni na camera tu. Josephati anasimulia hapa jinsi anavyojisikia “Nina maumivu makali sana, Mguu wangu wa kulia umepigwa na askari wapatao wanne, bega la kushoto nimepigwa na kirungu mara mbili. Mguu ulipigwa mateke matano ya nguvu, virungu na kusukumana, kisa ilikuwa ni amri haramu ya Paul Chagonja kuamuru askari wawafukuze watu wote wakiwemo waandishi wa habari wasiandike yaliyokuwa yanajiri kwenye tukio la kufika Mbowe kwenye makao makuu ya jeshi hilo. nimepitia ofisini niandike kwanza kilichojiri ndio niende hospitalini kutibiwa. Natembea kwa shida, imeniuma sana Umri tu ndio umesababisha nisilie. Chagonja alaaniwe, na walionipiga huku nikijieleza kuwa mimi Mwandishi, wakanipiga huku wakinitishia mbwa, na wao walaaniwe. Lakini sitaacha kupigania uhuru wa habari nchini ili watanzania wajue ushenzi wa askari wao na jinsi nchi yao inavyoendeshwa”
Isango 3Mtu mmoja (mwandishi wa habari) asiye na silaha yeyote akikabiliana na kipigo toka kwa askari watatu bila hatia yeyote.

9Askari wenye mbwa kabla ya kuwaruhusu mbwa hao wawaume raia

17Mwandishi aliyetambulika kwa jina moja tu la Badi, akilia kwa uchungu na kuwalalmikia Polisi kwa kitendo cha kumpiga vibaya na kumsakizia mbwa wakamuuma

5Mwandishi wa habari Shamim Ausi mmoja wa wanahabari walioumia na kupoteza fedha na mali nyingine

MwangosiHapa ni tukio la Daudi Mwangosi kuuawa na Polisi huko Iringa.

 

PICHA: VYANZO MBALIMBALI IKIWEMO GLOBAL  PUBLISHERS

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO