Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MASHAMBULIZI YA ANGA YA WAMAREKENI DHIDI YA ISIS NCHINI SYRIA

Majeshi ya Marekani yameanza rasmi mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria).Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya mchanganyiko kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono.Lakini habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji aliopo wa Raqqa ambako kuna makao makuu ya kundi hilo.
Mtu huyo anaetumia jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na drones.
Baadae Agency ya wanaharakati nchini Syria ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi.

Tazama video hapa chini (Kama simu yako haisomi player hii. Bonyeza >>>HAPA)

CREDIT: VIJANA NA MATUKIO BLOG

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO