Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi wa Nembo ya radio Triple A fm na kuwataka wamiliki na wanahabari kuhakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya uandishi wa habari iwe kazini au nje ya kazi zao.
Serikali imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia jamii bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa amani.
Naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia akiwa na Bodi ta wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Radio Triple A fM inayoongozwa na Mkurugenzi wake kulia na kushoto Mr&Mrs Papa King Mollel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya naibu waziri kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini hapa
Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
"Lengo hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na jamii"alisisitiza Nkamia
Kwa Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi aliwakemea mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo pia kupachika picha zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja
Baadhi ya viongozi wa serekali wa jiji la Arusha nao waliudhuria uzinduzi huo
Matindi alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata maadili hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka taaluma na weledi wa tasnia hiyo
Naye meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza Triple A Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa sekta mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii
Meya wa Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo akitoa nasaha chache kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa blue Frem uliopo kwenye klabu ya usiku ya TRIPLE A NIGHTY CLUB ya jijini hapa
Mkurugenzi wa The Blue Triple A Ltd Papaa King aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha kuwa Redio hiyo itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo kuwapa maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango .
Sehemu ya wafanyakazi wa Radio Triple A fm wakiwa katika picha ya pamoja kulia na kushoto kwa naibu waziri Nkamia ni Meneja wa redio hiyo Fredy Mumburi kushoto ni mkurugenzi wa redio hiyo Papa king molel baada ya uzinduzi wa logo ya redio hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki
Picha kwa hisani ya Libeneke la Kaskazini Blog
0 maoni:
Post a Comment