Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WANANCHI ARUMERU WABOMOA NYUMBA NA KUFYEKA MAZAO KWENYE VYANZO VYA MAJI

Vijana wakiwa na mabango kupinga uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.


Upandaji miti kwaajili ya utunzaji wa mazingira


Ubomoaji wa nyumba ukiendelea


Wananchi wakikagua chanzo kilichogeuzwa shamba


Arumeru.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki,wilayani Arumeru,wamebomoa nyumba moja iliyojengwa kwenye chanzo cha maji  ili kunusuru vyanzo hivyo ambavyo viko hatarini kukauka kutokana na ujenzi usiozingatia utunzaji wa mazingira.

Wananchi waliotekeleza hatua hiyo,Steven John na Frank Nnko walisema kuwa  wamechukua uamuzi huo baada ya serikali kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wa uvamizi wa vyanzo vya maji .

Nnko alisema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu kutokana na kuwa wananchi ndio waathirika wakubwa wa kukauka kwa vyanzo vya maji na kwamba  wameamua kujichukulia sheria mkononi na hawatasita kufanya hivyo kwa wananchi wengine watakaokiuka utunzaji wa mazingira.

Alifafanua kuwa kitongoji cha Momela ndicho chanzo kikuu cha maji katika Kata za King'ori,Makiba na Ngarenanyuki hivyo kuendelea kuwaachia wananchi wachache kuharibu mazingira kunaweza kugeuza eneo lote jangwa jambo ambalo linaweza kuhatarisha uhai wa watu na viumbe hai.

Mwenyekiti wa  jumuiya ya Maji bonde dogo  la Ngarenanyuki  ,Aminieli Mungure alisema kuwa vyanzo hivyo vimekua vikiharibiwa kwa  kukosa usimamizi hivyo wakati umefika wa jamii kuamka na kuvilinda kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aliongeza kuwa Bonde dogo la Ngarenanyuki linahudumia vijiji  vinne ambavyo ni Ngabobo, Olkung’wado,Uvizo na Ngarenanyuki na kuwa wataanza kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

 

CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO