Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI “JAMBO FESTIVAL” KUTIKISA ARUSHA

Wasaniiwa muziki wa asili wakitoa burudani katika tamasha la Jambo festival.

Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha  maarufu kama JamboFerstival   Augustine Michael Namfua

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa  na utamaduni la
kimataifa maarufu kama Jambo festival
litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili ,muziki wa
asili,mavazi na vyakula  ,tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la
Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.


Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi
wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani
na lenye kila aina ya ubunifu .


Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya,Rwanda,Burundi,Nchi za
Ulaya,Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa
ni wakazi wa Arusha.


Mwenyekiti wa Tamasha  la Jambo Festival , Augustine Michael Namfua
anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na
kwa sasa  linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.
Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo
lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.


Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na
utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania  na Afrika  kwa ujumla hasa
ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki
na ni mji wa utalii.


"Katika matamasha yetu kumekuwa na uwepo wa jamii ya kimataifa ambao
wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matamasha kwa njia ya mtandao na hata
kushiriki kwa wingi pia wapo wanaotuunga mkono" Alisema
Augustine


Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa lengo la tamasha hilo kukuza sanaa na
utamaduni,kukuza uchumi wa Arusha mathalani katika kipindi cha tamasha
watu kutoka kona mbali mbali za dunia watakuja na kulala,kula na
kununua bidhaa zinazotokana na utamaduni.
Vikundi mbali mbali vya ngoma vitatoa burudani ya kukata na shoka
katika tamasha hilo la aina yake.


Wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki watapanda jukwaani na
kutumbuiza mziki wa live utakaokonga nyoyo za mashabiki na wapenzi
watakaojitokeza katika tamasha hilo ambapo kundi la Jambo Squard
wanaotamba na nyimbo ya Mamong'o watatoa burudani.


Wasanii wengine ni kama Santuri DJs CAB (kutoka Ufaransa), Damian
Soul, Christian Bella,DJ Kahlil, Msafiri Zawose, Jambo Squad, Maia Von
Lekow, Warriors from The East,Aqua Sound Band, Hisia,Jhikoman &
Afrikabisa Band, Heart Band, G Nako kutoka WEUSI,Nash MC,
Chaba,Shamsila.


Pia kutakua na maonyesho ya mavazi ya kitamaduni ambapo yataandaliwa
na wabunifu mashuhuri ambao watakuwepo ikiwamo  Ally Rehmtullah, Diana
Magesa,Salim Ally,Martin Kadinda,Nahuja Nuhu,Neema Meena,Zakia Ally.
Vile vile Kutakuwa na vyakula vya asili kutoka makabila mbali mbali ya
Tanzania na Afrika Mashariki pamoja na nchi washiriki bila kusahau
Nyama choma.


"Arusha ni mji unaosifika kwa nyama choma katika tamasha hili
tumejiandaa vyema watu wafike wapate nyama choma nzuri na vinywaji
huku wakifurahia mziki wa asili unaopigwa live" Alisema


Kwa upande wa kiingilio ni bure kwa nyakati za mchana na baada ya hapo
jioni watatakiwa kulipa shilingi 5000 kama kiingilio  ambacho
kinasaidia tamasha kuendesha shughuli zake.kutakuwa na sehemu mbili
mchana na usiku.


Tamasha la Jambo Festival litafanyika jijini Arusha katika viwanja vya
Nane Nane vilivyopo eneo la Njiro jijini Arusha ,  litaanza siku ya
ijumaa tarehe 3 hadi 5 octoba mwaka huu.Watu wote wanakaribishwa
kufurahia sanaa na utamaduni ambayo ni burudani isiyo na kifani.
Jambo Festival itapambwa na ngoma za utamaduni,muziki wa
jukwaani,vyakula vya asili,soko za sanaa za mikono pamoja na michezo
ya watoto.


Tamasha hilo limedhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa,Kituo cha Utamaduni
cha Ufaransa na wadhamini wengine na kuandaliwa na shirika la Idea
Afrika.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO