Mkuu wa kitengo cha sheria CHADEMA, Tundu Lisu, (Katikati), akiongozana na washtakiwa kwenye kesi ya kukusanyika isivyo halali wakati wakitoka mahakama ya wilaya ya Dodoma Jumanne Septemba 23, 2014. Lisu ambaye alikuwa akiwatete washtakiwa hao ambao baadhi yao ni viongozi wa chama hicho mkoani Dodoma, alisema, walishtakiwa kwa kosa la kukusanyika isivyo halali hapo Septemba 18, mwaka huu,wiki iliyopita na waliachiwa huru kwa dhamana.
Lisu akiongozana na washtakiwa wakati wakitoka mahakani hapo, Jumanne Septemba 23, 2014
***********************************************
HABARI YA GLOBAL PUBLISHERS: Mahakama ya Kisutu yawaacha wafuasi wa Chadema waliokamatwa kwa kumsindikiza Mbowe!
Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi hivi karibuni.
Na Mwandishi wa GPL
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru kwa dhamana washitakiwa watatu wenye kesi namba173 ya mwaka 2014, kwa kosa la kumsindikiza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Makao Mkuu ya Polisi.
Washitakiwa hao ni Ngaiza Kamugisha ambaye ni mfuasi wa chama hicho, Katibu wa BAVICHA Temeke, Benito Mwapinga na Elisante Bagenyi ambae ni mfuasi wa chama hicho, walifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa dhamana kufuatia maombi yaliyopelekwa na wakili wao John Mallya.
Akisoma mashitaka hayo, mbele ya Hakimu mkazi Frenk Moshi, Wakili wa serikali Benard Kongola alidai kuwa mshitakiwa huyo namba moja mwenye miaka (28), mkazi wa Vingunguti alikuwa anakabiliwa na kosa la kutoa lugha chafu na kukiuka amri za jeshi hilo alipokuwa makao makuu.
Alisema kufuatia maombi hayo, washitakiwa wengine wawili ambao walitenda kosa hilo hilo nao waliachiwa juzi kwa dhamana ya sh. mil.5 kwa kila mmoja, huku mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Kamugisha alirudishwa rumande na kutolewa jana kwa dhamana ya kiasi hicho.
Alisema kuwa, kosa hilo alilitenda mnamo Septemba 18 mwaka huu, majira ya saa 11 asubuhi, katika maeneo hayo ambapo lilitolewa onyo kuwa mtu asivuke eneo hilo kutokana na taratibu za kiusalama.
Kwa mujibu wa Kongola, Kamugisha alitumia lugha chafu kwa maafisa wa Jeshi la polisi akiwemo Insipekta Zuhura, ambapo kauli hizo zingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
0 maoni:
Post a Comment