Waandishi wa habari wakirekodi tukio la kuwasili kwa Mh. Freeman Mbowe (hayuko pichani) Makao Makuu ya Polisi.
Mh. Tundu Lissu akiwasili. Mbuge wa Ubungo, Mh. John Mnyika akiwa ndani ya gari baada ya kukataliwa kuingia. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mh. Wenje (kushoto), Mh. Msigwa na Mh. Joseph Mbilinyi wakiingia katika jengo hilo. Mwandishi wa habari Shamim Ausi mmoja wa wanahabari walioumia na kupoteza fedha na mali nyingine. Wanachama wa Chadema wakiwa wamekalishwa chini na askari. Kina mama ambao ni wanachama wa Chadema waliofika makao makuu ya polisi. Polisi wakiwakimbiza waandishi wa habari (hawako pichani) kwa kutumia mbwa. Wanahabari wakiwa mekusanyika baada ya kutimuliwa na mbwa. Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi.
Muonekano wa polisi katika tukio hilo. Askari wakiwa hawataki kuwaona wanahabari eneo hilo.
Mwandishi wa habari, Badi, akilia kwa uchungu baada ya kuumizwa na mbwa wa polisi.
MNYIKA, WANASHERIA WAZUIWA KUINGIA NDANI WANAHABARI WAKIMBIZWA NA MBWA, WAUMIA, WAMWAGA MACHOZI
MAMIA ya watu wamejitokeza leo kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam kuhusiana na kauli yake aliyotoa majuzi juu ya kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.
Kilichofuata ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa umbali wa mita 200 ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao waliumia na kupoteza zana zao za kazi.
TAARIFA NA PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS LTD
0 maoni:
Post a Comment