"Tanga mmeendelea kuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu mmeendelea kukikumbatia Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwapigia kura na kuwafanya wawatawale kwa muda mrefu bila kuwaletea maendeleo, nimesikiliza risala hapa mnahitaji Shule, umeme, maji salama, zahanati n.k vitu ambavyo mikoa inayoongozwa na Upinzani wamesahau, kama ni shule labda wanataka kujenga shule ya nne au zaidi"
Hayo yamesemwa leo Jumamosi 25/03/2017 na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Freeman Mbowe akiwa katika ziara mkoani Tanga ambapo amezindua ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Muheza na kuzindua msingi wa Chama katika kijiji Mpakani Kata ya Kwa Kifua Muheza Tanga.
Hii ni muendelezo wa ziara katika Kanda zote 8 nchini, Ziara hii imeshapita katika Kanda ya Nyasa, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Pwani na sasa ni Kanda ya Kaskazini ambayo inajumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Dhumuni la ziara hii ni kuwashukuru wananchi/ wapenzi/ wakereketwa wa CHADEMA, kuangalia uhai wa Chama mara baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba 2015, kuongea na viongozi katika ngazi kupitia mikutano ya ndani, kuvuna wanachama wapya, kuzungumzia na kuleta Ujumbe wa Chama kuhusu hali ya siasa, uchumi nchini pamoja na kukijenga Chama n.k .
CHADEMA ina utaratibu wakuwashukuru wananchi kila baada ya Uchaguzi unapomalizika, kwa niaba ya mgombea Urais Mhe. Lowassa, Mhe. Mbowe amewashukuru sana wananchi wa Muheza.
0 maoni:
Post a Comment