Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wanachadema 6 Waliokamatwa Ijumaa Wakimpokea Lema Alipopata Dhamana Wapandishwa Kizimbani

Wakili Sheki Mfinanga akiwa na baadhi ya waliokamatwa na kufikishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya fujo.  Wote walikamatwa kutoka ndani ya gari walizokuwamo katika msafara wa kumsindikiza Mbunge lema nyumbani kwake mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.


Wakili Sheki Mfinanga akiwa ndani ya chumba cha Mahakama

Ndani ya Ukumbi wa Mahakama ya Moromboso, watuhumiwa wakisubiri kusomewa shitaka

Watu sita wanaodhaniwa kuwa wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, akiwemo Dereva wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa ndugu Allan Bhujo, Dereva wa Chadema Kanda ya Kaskazini Alexander Kapalale, mpiga picha wa Mhe.Mwenyekiti wa Chadema Taifa ndugu Dominick Mgaya pamoja na makamanda wengine watatu waliokamatwa siku ya Ijumaa tarehe 03.03.2017 mara baada ya Mbunge wa Arusha Mjini kuachiwa kwa dhamana, wamepandishwa kizimbani leo, Mahakama ya Mwanzo Moromboso jijini Arusha na kuachiwa  kwa dhamana ya Sh laki 6 kufuatia shtaka lakufanya fujo, ambapo washtakiwa wote 6 wamekana shtaka hilo.

Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Mongi ameihairisha kesi hiyo na itatajwa tena tarehe 17.03.2017.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO