Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MJENGONI BANDI KUFANYA UZINDUZI RASMI MARCH 3 KATIKA UKUMBI WA TRIPLE A SPORT BAR


 wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu

Rais wa bendi ya mjengono Robert Mukongya (Digital) akiwa anaimba ndani ya jukwaa  


Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Bendi mpya  ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni   classic   band inatarajia kufanya  utambulisho   wao rasmi kwa mara ya kwanza  mapema  march 3 katika ukumbi wa Triple A spot bar uliopo ndani ya jiji la Arusha

Akiongea na waandishi wa habari  Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa  pamoja kuwa bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi  hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi katika siku hiyo ya alyamisi.

Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na  wanamuziki wa bandi ya mjengoni

Kwa upande wake  mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdeme alisema kuwa bendi yake imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha  waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.

Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya jirani kuhuthuria onyesho hilo  kwani bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.

Alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa mbili usiku adi majogoo  ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO