Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kikao cha Kwanza 2017: Halmshauri ya Jiji la Arusha Yaidhinisha Mpango Kabambe wa Kuboresha Jiji

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akiteta jambo na Naibu wake Mh Viola Likindikoki katika kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo kilichoketi jana kujadili na kuidhinisha mambo mbalimbali.  

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh Hamis Kihamia akizungumza katika kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo kilichoketi jana kujadili na kuidhinisha mambo mbalimbali.  

Waheshimiwa madiwani na wajumbe wengine wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha wakiwakwenye kikao jana. 

Diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro akichangia jambo kuhusu hoja ya kuurejesha uwanja wa Sheikh Amri Abeid chini ya umiliki wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. 


MAELEZO YA ZIADA NA AFISA HABARI WA JIJI
Kikao cha Baraza la Madiwani Jiji la Arusha kilichoketi kwa robo ya pili kwa mujibu wa kanuni kimepitisha taarifa mbalimbali za shughuli za maendeleo, kuidhinisha mapendekezo ya Sheria ndogo za Jiji za mwaka 2016 pamoja kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Taasisi za Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi wa Jiji la Arusha.
Akifungua Kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro amewataka wajumbe wa Kikao kuwa makini katika kujadili na hoja mbalimbali zilizowasilishwa katika Baraza ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi wa Jiji na wanaotegemea kupata maendeleo kupitia vikao.
Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia alisema kwa kushirikiana na Menegiment amehakikisha kwamba maazimio yote ya vikao vya awali yamezingatiwa na miradi imetekelezwa kwa kiwango cha juu huku thamani ya Fedha ikionekana.
Kutoka katika taasisi zilizoalikwa katika kikao hicho Mkurugenzi wa AUWSA Eng Ruth Koya alieza changamoto kubwa inayowakabili wananchi kwa sasa kuwa ni uhaba wa Maji na kusema kuwa wanategemea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utawezesha upatikanaji wa maji Lita Mil 200 wakati mahitaji ni Mil 94 tofauti na sasa ambapo kiasi kinachohitahjika ni Lita Mil 35 tu ambacho hakitoshelezi hata nusu ya mahitaji ya wananchi, hivyo kinachohitajika ni ushirikiano wa wadau na wananchi ili kuweka kufanikisha utekelezaji.
Akiendelea kujibu maswali ya Wah. Madiwani waliyohoji maji yanayopatikana kuwa na Chumvi Eng. Koya alisema maji ya kisima yanayopatikana Arusha kwa kiasi kikubwa yana uwekezekano wa kuwa na chumvi kidogo lakini na hayana Flouride tofauti nay ale ambayo wananchi wanadai ni matamu huwa ni ya yanatokana na Chemchem ambayo hayapatikani kwa wingi na athari zake ni kuwa na Flouride ambayo mtumiaji huwezi kuigundua kwa kunywa lakini athari zake huonekana kwenye meno nk.
Kutoka Tanesco Mhandishi wa Mipango na Ubunifu Eng.Beatus Rwegoshora alifafanua tatizo la kukatika umeme mara kwa mara kuwa Tanesco iko katika maboresho ya huduma kwa wateja nahivyo tatizo hilo litapungua na pia shirika lipo katika mpango mahususi wa kuwafanya wananchi waweze kupata taarifa zote za msingi kupitia simu za kiganjani ambapo huduma hiyo itawafanya wananchi kufuatilia na kupata taarifa kwa wakati na muda wote popote walipo.
Meneja wa Sumatra Mkoa wa Arusha Bw. Allen Mwani amesema kwa sasa Mamlaka hiyo ipo katika upembuzi yakinifu wa mradi wa kuondoa usafiri wa daladala maarufu, 'Vifodi' ambazo hazina viwango katika usafirishaji wa abiria hivyo mpango uliopo ni wadau kukaa pamoja na kuleta magari makubwa ya usafirishaji wa abiria(City Bus) katika jiji la Arusha.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala AICC Ndg. Savo Mng’ong’o aliwatoa shaka Madiwani waliolalamikia Hospital ya Kituo hicho kutopokea Kadi za Bima ya Afya (NHIF) ilihali wananchi wanahimizwa kujiunga na mfuko huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa alifafanua kuwa huduma hiyo itarejea mwezi Oktoba.
Katika kikao hiki pia Baraza limepitia na kuidhinisha Sheria ndogo za Halmashauri ambapo sasa zitawasilishwa Mkoani kisha Tamisemi kwa ajili ya kuidhinisha kisha kuanza kutumika rasmi. Sheria hizi ni muhimu sana kwa jiji kwa kuwa zinazotumika sasa ni zile za mwaka 2003.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO