Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NGUO MAURITIUS


 Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha kuengeneza nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee kilichopo nje kidogo ya mji wa Port  Louis nchini Mauritious. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo zilizoshonwa  kwa vitambaa vilivyotengenezwa na kwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee cha Mauritius wakati alipotembelea kiwanda hicho, nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini Mauritius, Machi 22, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza viongozi wa kiwanda cha  nguo cha Mauritius cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis Machi 22, 2017.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.

Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini Tanzania na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi pamoja na nguo kwa kuwa kuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.

Waziri Mkuu alitembelea kiwanda hicho kilichoko katika mji wa Latour Koenig jana (Jumatano, Machi 22, 2017) na kujionea namna wanavyotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuamua kuwakaribisha waje kuwekeza nchini.

“Tumefarijika na uwekezaji wenu na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nvingi na yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.

Waziri Mkuu alisema madhumuni  ya kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika  viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na kuwawezesha wakulima kupata tija.

“Tunalima pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi ”  alisema.

Alisema viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato.

Mbali na kuwakaribisha wawekezaji hao, pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya kuiuza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho Bw. David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.

Bw. David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200. “Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka makubwa barani Ulaya,”

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 23, 2017.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO