Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mohammed Dewji ashinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bora Afrika 2017


Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa mwaka 2017 inayotolewa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Afrika (Africa CEO Forum). Dewji ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda Abdulsamad Rabiu (CEO wa BUA Group), Issad Rebrab (CEO wa Cevital), Naguib Sawiris ( CEO wa OTMT Investments), Said Salim Awadh Bakhresa (CEO wa Bakhresa Group) na Strive Masiyiwa (CEO wa Econet). Akizungumza kuhusu ushindi huo, Dewji ameishukuru Africa CEO Forum kwa kutambua mchango wake kwa kumchagua kuwa mshindi tuzo hiyo lakini pia kuwashukuru Watanzania na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya kudhibiti na kubana matumizi mabaya ya pesa ya umma. “Ninashukuru sana Africa CEO Forum kwa heshima hii ambayo mmenipa, napenda kutoa tuzo hii kwa nchi yangu Tanzania, bila wao nisingekuwa hapa na MeTL Group isingekuwa katika nafasi iliyonayo sasa, nawashukuru sana kwa kuniruhusu mimi na familia nzima ya MeTL kukua na kufika hapa, “Pia napenda kutoa heshima kwa Rais wangu John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri na wote tunajua Afrika inavyokabiliwa na vitendo vya rushwa lakini yeye ni mmoja wa watu ambao wanapambana na rushwa, kubana matumizi mabaya na wenye mwono katika kazi yake.” alisema Dewji. Aidha Dewji alisema kwa sasa bara la Afrika uchumi wake unakua kwa kasi huku akitolea mfano wa ripoti yam waka 2015 ambayo ilionyesha uchumi wa Afrika unakua kwa asilima 4 kwa mwaka kulinganisha na Ulaya inayokua kwa asilimia 1.5 hivyo kuwashauri wanachama wa Afrika CEO Forum kutumia vyema fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi. Washindi wengine wa tuzo zilizotolewa na Africa CEO Forum ni; CEO of the Year
  • Abdulsamad Rabiu, CEO, BUA Group
  • Issad Rebrab, Chairman, Cevital
  • Mohammed Dewji, CEO, MeTL - WINNER
  • Naguib Sawiris, Chairman, OTMT Investments
  • Said Salim Awadh Bakhresa, CEO, Bakhresa Group
  • Strive Masiyiwa, CEO, Econet
Young CEO of the Year
  • Anta Babacar Ngom Bathily, DG, Sedima - WINNER
  • Basil El-Baz, PDG, Carbon Holdings
  • Darshan Chandaria, PDG, Chandaria Industries
  • James Mworia, PDG, Centum Investments
  • Mohamed Ben Ouda, DG, SNTL
  • Lamia Tazi, DG, Sothema
African Company of the Year
  • CIEL Group
  • ECONET
  • Elsewedy Electric - WINNER
  • Label’Vie
  • MTN
  • OCP Group
African Bank of the Year
  • Attijariwafa Bank - WINNER
  • Banque Centrale Populaire
  • Ecobank
  • Mauritius Commercial Bank
  • Standard Bank Group
  • . United Bank For Africa
Private Equity Investor of the Year
  • Actis
  • Afrinvest - WINNER
  • Development Partners International LLP
  • Helios Investment Partners
  • Leapfrog Investments
  • The Abraaj Group
International Corporation of the Year
  • Allianz - WINNER
  • Coca-Cola
  • Mota-Engil
  • Orange
  • Siemens
  • Vitol
Tuzo za Africa CEO Forum zimetolewa Geneva, Switzerland ambapo wanachama wa jukwaa hilo wapo katika mkutano wa siku mbili wakijadili mambo mbalimbali ambayo yanawahusu wao kama Watendaji Wakuu na jinsi gani wanaweza kulisaidia bara la Afrika.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO