Muuandaaji ya wiki ya wanawake duniani kwa mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo vya afya yake
Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro akiwa anaingia uwanjani tayari kwa uzinduzi Rasmi zoezi la kupima Moyo, Cancer, Kisukari, Macho, Magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa Bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani tar 8/3/2017
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Tatizo la baadhi ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari ,kansa,na shinikizo la damu.
Tatizo la baadhi ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari ,kansa,na shinikizo la damu.
Hayo yalisemwa na mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt meru,Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Akihojiwa na waandishi wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai kuwa mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa hayo.
“mtindo wa maisha umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye mazoezi na kuzingatia mlo wenye utaratibu”alisema mtaalamu huyo
Hatahivyo,mtaalamu wa magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani kilimanajro,DK Valeria Matei alisema kwamba katika siku za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na wazee ambao ilikuwa imezoeleka.
Alisema kwamba elimu ya afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.
Doroth Kuziwa, ambaye ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe kumudu gharama hizo.
Hatahivyo,Hiza Omary ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika jamii.
Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment,Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia mkataba na hospitali za KCMC na Mt Meru kwa lengo la kufadhili zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa mkoa wa Arusha katika kuelekea siku ya wanawake duniani.
Alisema kwamba zoezi hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa.
mmoja wa madaktari wanaotoa huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye amejitolea kuchangia damu
mmoja wa daktari akimpongeza mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa presha
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa bure
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya mfumo wa Hewa .. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi Mkoani Arusha
mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo mara baada ya kuzindua wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
0 maoni:
Post a Comment