Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Madaktari Kenya Waapa Kutorudi Kazini

Madaktari wanaogoma wamesisitiza kuwa hawatarudi kazini hadi serikali itakapotia saini mkataba wa makubaliano.Madaktari  hao  hata hivyo  wanasema wako tayari kuendelea kushauriana na serikali ili kuafikiana kuhusu maswala chache yanayoibua utata, ili kumaliza mgomo huo ambao umedumu kwa miezi mitatu sasa.Lakini katibu mkuu wa chama cha madaktari na watalaamu wa meno Dr Ouma Oluga kwenye kitandazi chake cha twita  ameelezea kughadhabishwa na kwake, na kile ametaja kuwa vitisho kutoka kwa serikali,akisema madaktari hawapigani na serikali, bali wanashinikiza  kuboresha kwa sekta ya afya hapa nchini  kwa jumla, kwa manufaa ya Wakenya wote.  Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha madaktari –KMA Jacqueline Kitulu amevikosoa vyombo vya habari kwa kutoa habari za kupotosha kuhusu nia ya mgomo wa madaktari.Alisema vyombo vya habari vinaangazia tu swala la nyongeza ya mshahara, ilhali kuna maswala mengine muhimu yanayoshinikizwa na madaktari kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.Kitulu amesema hayo huku serikali ya kitaifa na za kaunti zikiendelea kuwafuta kazi madaktari waliopuuza agizo la kurejea kazini.Hadi sasa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imewafuta kazi madaktari 12,huku hospitali nyingine kadhaa pia zikijiandaa kufanya hivyo.
CHANZO: KBC
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO