Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGA


RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGATanga, MKUU wa  Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino  cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.
Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri huduma.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa
Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.
Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.  Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange  kupunguza kero ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange  Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati  350 yaliyotolewa  na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangakumekucha
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO