Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Chadema Kalenga Waishutumu CCM Kumjeruhi Kijana Mmoja Kwa Kisu Kwenye Moyo Baada Ya Mama Yake Kuhamia Chadema

IMG-20140308-WA0043

IMG-20140308-WA0034Ikiwa siasa za vurugu zikionekana kuwa sehemu ya utamaduni wa siasa zetu bila ya Serikali na Vyombo vya usalama kuzuia mbegu hiyo mbaya isienee, kumeibuka tuhuma nzito dhidi ya CCM kumjeruhi vibaya kijana mmoja wa Chadema aliyekuwa nafanya kampeni za nyumba kwa nyumba jioni

Kijana huyo pichani, Richard Mawata alinusurika kifo juzi baada ya kuvamiwa na kundi la watu sita na kuchomwa na kisu eneo la kifua jirani na moyo.

Inaeleza kuwa walimvizia mahali akitoka kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuhamasisha watu kumchagua mbunge mtarajiwa na kuhudhuria mkutano wa Luhota. Wakamvizia wakati anakwenda nyumbani mahali ambapo hakuna watu wala nyumba akiwa na baiskeli yake wakasimama mbele yake kuziba njia, alipofika tu wakamshambulia na kumchoma kisu. Alilazimika kupata msaada wa wasamaria wema pamoja na viongozi wa Chadema waliowahi kufika eneo la tukio kwenda hospitali.

IMG-20140308-WA0014

Richard Mawata akiugulia kwa maumivu makali wakati akipatiwa matibabu. Blog hii imefahamishwa kuwa Richard alikuwa  kiongozi wa Baraza la Vijana la CHADEMA na alichomwa kisu usiku wa kuamkia jana na mama yake mzazi alikuwa ni kiongozi wa Serikali ya Kijiji kabla ya kuhamia Chadema.

Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Mama mzazi wa kijana aliyechomwa kisu alikuwa amejiunga Chadema juzi, ambapo baada ya masaa machache kujiunga na Chadema, mtoto wake akakutwa na dhahama hiyo ya kuchomwa kisu karibu kabisa na kwenye moyo.

IMG-20140308-WA0077 Pichani ni mama mzazi wa kijana aliyechomwa kisu akipongezwa na Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar huku Meneja Kampeni akishuhudia, mara baada ya kuamua kujiunga na Chadema.

Picha na Tumaini Makene, Afisa Habari Chadema.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO