Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Namna Rais Uhuru Kenyata alivyoondoka Kenya kuelekea Arusha kwa Gari..Afungua EALA leo Jijini Arusha

KENYA_6

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta jana alisafiri kuelekea mkoani Arusha nchini Tanzania kwa usafiri gari kwa njia ya barabara, safari ya umbali wa kilometa 230.
Rais Kenyatta alisimama katika maeneo kadhaa kabla ya kuvuka mpaka wa Namanga kwa kutumia kitambulisho kipya kinachoruhusu wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia kusafiri baina ya nchi hizo kwa urahisi.
Akiwa Arusha, Rais Uhuru atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako atapokelewa na katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera.
Siku ya Jumanne anatarajiwa kulihutubia bunge la Jumuiya hiyo kwa wadhifa wake wa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa sasa. Anatarajiwa kusisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Credit: HabariKwanza Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO