Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais Jakaya Kikwete awaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma.

 

IMG_4232

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Yahya Khamis Hamad akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Katibu bunge Bw. Yahya Khamis Hamad (mbele aliyesimama)

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akipokea vitabu vya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.

Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Naibu Katibu bunge Maalum la Katiba Bw. Thomas Kashilila (aliyesimama)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwaeleza jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia kwa Rais) akifuatiwa na  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta, Prof. Mark Mwandosya na Mwisho Pindi Chana.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta (kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho wakati wa Hafla ya kuwaapisha Katibu na Makamu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Mwenye tai ya bluu) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia), Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. na Naibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila (Kushoto kwa  Katibu wa Bunge) Leo Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimweleza jambo Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Juma Nkamia wakati wa Hafla ya Kuapishwa kwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma.  (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO