Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

GK atangaza ujio mpya wa East Coast Team

east_7MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Gwamaka Kaihula ‘King Crazy GK’ amewataka wapenzi wa kundi la muziki huo la East Coast Team kukaa mkao wa kula baada ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo kujipanga kurudi upya.

Baadhi ya wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo ni Ambwene Yesaya ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, mwanadada Judith Wambura ‘Jide’ na GK.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, GK alisema, huu ni wakati wao wa kufanya kazi kama zamani kwa kutoa burudani nzuri ambazo zimekwenda shule.

“Tumeanza kuongeza nguvu katika kundi letu jipya, tunatakiwa kufanya kitu kipya katika kiwango cha juu vitu ambavyo watu hawataamini kama ni sisi,  tunatakiwa kuwa katika viwango vingine kwasababu tukiwa katika hali ilele inamaana kutakuwa hakuna maana ya kurudi upya,” alisema GK.

Alisema wameshapata studio ya kimataifa ambayo itatumika kutengenezea kazi zao, na kwamba kwasasa ataanza kutambulisha kazi yake ambayo ameshirikiana na AY na Mwana FA.

GK alishawahi kutamba na ngoma zake kama ‘Baraka au Laana’, ‘Leo’ na nyinginezo nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Chanzo: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO