Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UPANUZI WA MITAMBO YA RUBU KUWASAHAULISHA WAKAZI WA DAR NA ADHA YA MAJI

SONY DSC

Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.

SONY DSCTimu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.

SONY DSCKaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.

SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.

SONY DSCMeneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.

SONY DSCViongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.

SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).

SONY DSCTimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.

Picha na Saidi Mkabakuli

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO