Viongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Wanne Kushoto aliyenyanyua mkono) na Bibi Florence Mwanri (Watatu Kushoto) wakipata maelekezo ya Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Pichani ni ujenzi wa sehemu wa kukaa abiria ukiendelea.
Meneja uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya, Eng. Valentino Kadeha (Kulia) akitoa maelekezo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea Mradi huo. Kwa Mujibu wa Mhandisi Kadeha Uwanja huo umeshakamilika kwa aslimia 70 na utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria zaidi ya 300 kwa saa.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr Sankey (Wapili Kulia) akieleza changamoto zinazozikabili Hospitali hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilipotembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Aliyeambatana nae ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Humphrey Kiwelu (Kulia).
Naonja Maji.. Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye nguo nyeusi) akionja maji kutoka moja ya njia za kusambazia maji ya Mradi wa Maji wa Iwalanje. Kukamilika kwa Mradi huo kumetoa suluhisho la adha ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Kijiji cha Iwalanje na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazohudumiwa na Mradi huo.
Ukaguzi wa Hospitali.. Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa maendeleo ya nchi, Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilitembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Timu hiyo ilishuhudia maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kitengo cha Dharura (linaloonekana nyuma).
Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) akipata maelezo ya maendeleo ya Mradi wa Maji ya Mtiririko Kijiji cha Igurusi kutoka kwa Mshauri wa Mradi huo Mhandisi Kimambo.
Wakaguzi walipata bahati ya kujionea chanzo cha maji hayo kutoka nje kidogo ya Kijiji cha Igurusi.
Kikazi Zaidi.. Timu ya ukaguzi pia ilikagua maendeleo ya Tanki la kuhifadhia maji la mradi huo. Pichani, Kiongozi wa Ukaguzi, Bibi Florence Mwanri akipanda ngazi kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa Tanki.
DSC04343
Ujenzi unaendelea.. Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi huku wakaguzi hao wakikagua. Tanki hilo lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki tano ambalo limeshakamilika kwa asilimia 90. Hadi kukamilika kwake Mradi utagharimu jumla ya Shilingi zaidi ya Milioni 830.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Aliyenyanyua Mkono) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Maji wa Iwalanje wakati Timu ya Ukaguzi ilipotembelea Mradi huo.
Timu ya Ukaguzi pia ilishuhudia Tanki la kuhifadhia maji la Mradi huo lenye uwezo wa kuhifadhi lita 43,000. Mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi milioni 273, ambapo mpaka sasa Mradi unahudumia zaidi ya kaya 2, 506.
Picha zote na Saidi Mkabakuli
0 maoni:
Post a Comment