Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE CHA JIJINI ARUSHA

DSC02997

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakitazama bidhaa zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho kilisimama uzalishaji tangu mwaka 2007.

DSC02964

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyeusi) akioneshwa moja ya mashine zilizokuwa zinatumika kutengenezea matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichopo katika jiji la Arusha na Mwangalizi wa Kiwanda hich, Bw. Leonald Mgoyo. Serikali ina mpango wa kukifufua kiwanda hicho baada ya kusimama uzalishaji tangu mwaka 2007.

DSC02931

Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha

DSC02992

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakifurahia jambo wakati wa ukaguzi huo.

DSC02988

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyusi) akiagana na Mwangalizi wa Kiwanda hicho, Bw Leonald Mgoyo baada ya ukaguzi wa kiwanda hicho. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Gideon Nasari na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uzalishaji, Bw Maduka Kessy.

Picha na Joyce Mkinga,

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO