Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Police Family Day ilivyofana Jijini Arusha; Tozo la Notification Lafikia Tsh. 2,025,540,000/= kwa mwaka

Imeelezwa kwamba jukumu la kulinda amani na usalama wa nchi ni la kila mtanzania yeyote awe anaishi humu nchini au nje

ya nchi. Hayo yameelezwa na Mdau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Bw. Faisal Juma Shahbhai wakati wa sherehe ya Siku ya Familia za Polisi Mkoa wa Arusha katika kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika wiki hii katika ukumbi wa Hoteli ya Naura iliyopo jijini hapa.

Bw. Faisal alisema kwamba yeye na wanajamii wengine hawapaswi kukaa pembeni na kuliacha suala la ulinzi kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama pekee bali wao wanatakiwa wawe watu wa kwanza katika kukabiliana na uhalifu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwapa taarifa za mara kwa mara.

Mdau huyo aliongeza kwa kusema, ni vema kila mtu akatambua kwamba, kama yeye hajaathiriwa na matukio ya uhalifu basi ndugu yake au rafiki yake atakuwa amekumbwa na matatizo kutoka kwa wahalifu hao. Alisema ifikie wakati sasa jamii ijitoe kwa hali na mali katika kushirikiana na Jeshi la Polisi ili takwimu ya vitendo vya uhalifu izidi kupungua siku hadi siku.

“Ulinzi unaanza na wewe pamoja na mimi sio huko juu kwani ndio ambao tunawafahamu wahalifu hivyo kila mmoja atambue majukumu yake ndani ya nchi na anatakiwa awaze naye ameifanyia nini nchi yake”. Alisema Bw. Faisal.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, Jeshi la Polisi Mkoani humu lilifanya vizuri sana katika kupunguza vitendo vya uhalifu mwaka 2013 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Alisema mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi hilo na wananchi hivyo kutokana na hilo alimshukuru kila mmoja kutokana na mchango wake katika kuimarisha amani ndani ya Mkoa.

Alisema Jeshi hilo Mkoani hapa litaendelea kufanya kazi kwa weredi na kutoa huduma bora kwa mteja wa ndani na wa nje hali ambayo itasaidia ustawi wa mahusiano bora baina ya wananchi na Jeshi hilo na hivyo kupata taarifa zaidi za uhalifu na wahalifu.

Kamanda Sabas aliwaomba wanasiasa waendelee kutoa ushirikiano zaidi kwa jeshi hilo kwani wao ni watu muhimu sana katika kuimarisha amani ndani ya mkoa huu.

Aidha akitoa takwimu za Usalama Barabarani alisema jeshi hilo mwaka 2013 limepunguza ajali hizo kwa asilimia 52.8 ikilinganishwa na mwaka 2012 lakini pamoja na mafanikio hayo tozo la notification limeongezeka toka Tsh. 1,245,520,000/= mwaka 2012 hadi kufikia Tsh. 2,025,540,000/= mwaka 2013

pi1

PICHA YA PAMOJA YA WANA KAMATI YA MAANDALIZI YA SHEREHE WAKIWA PAMOJA NA MEZA KUU.

MGENI RASMI AMBAYE ALIKUWA NI MKUU WA WILAYA YA ARUMERU BW.NYIREMBE MUNASA AMBAYE ALIKUWA ANAMUWAKILISHA MKUU WA MKOA WA ARUSHA AKISALIMIANA NA WAGENI MBALIMBALI HUKU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA (SACP) LIBERATUS SABAS AKIWA PEMBENI YAO

BAADHI YA WANAMTANDAO WA ASKARI WANAWAKE TPF NET WAKITOA ZAWADI KWA ALIYEKUWA MWANACHAMA MWENZAO INSPEKTA KIVUYO AMBAYE AMESTAAFU HIVI KARIBUNI

KAMATI IKIWA TAYARI KUKARIBISHA WAGENI WAALIKWA

BAADHI YA WANAKAMATI WALIOFANIKISHA SHEREHE YA POLICE FAMILY DAY ILIYOFANYIKA KATIKA HOTEL YA NAURA ILIYOPO JIJINI ARUSHA

Makamu mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya sherehe Polie Family Day Bw. Faisal Juma Shahbhai akitoa neno kwa wageni waalikwa

SOURCE: LIBENEKE LA KASKAZINI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO