Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAPACHA WANNE WALIOZALIWA JIJINI MBEYA WAENDELEA KUKUA VIZURI

MAPACHA

Mapacha wanne kutoka kulia ni Asifiwe, Daudi,Anania na Alinikumbu wakionesha nyuso za furaha ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa afya zao.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha mpumpi kijiji cha Chiwanda, Winston Mtali akipokea msaada kwa niaba ya Familia kutoka kwa Joseph Mwaisango moja ya Wakurugenzi wa mbeya Yetu Blog kwa niaba ya Kampuni ya Michuzi Media waliofanikisha misaada hiyo kutoka Uingereza.

Erick Mwaisango akimkabidhi moja ya zawadi Mama Wanne kwa niaba ya Kampuni yaNora SilverBoutique ya Jijini Dar Es Salaam.

Familia ya mama wanne ikiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kijiji na kitongoji baada ya kupokea Msaada  kutoka kwa Wasamaria wema waliowakilishwa na Joseph na Erick Mwaisango.

Baba Wanne Webson Simkanga na mkewe Aida Nakawala wakiwa wamewabeba watoto wao.

Wanahabari Venance Matinya wa gazeti la Jamboleo na Ezekiel Kamanga wa Bomba fm Redio wakichukua maoni kutoka kwa Baba Wanne.

 

Baba na Mama wanne wakifurahia misaada iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia yao.

Baada ya kuwasili nyumbani kwa Mama Wanne, Moja ya wakurugenzi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango ambaye alikuwa ni kiongozi wa Msafara akionesha baadhi ya zawadi zilizopelekwa.

Baadhi ya watoto na wakazi wa kijiji cha Chiwanda wakisaidia kushusha mizigo kwenye gari huku wakionesha kufurahia misaada hiyo.

WATOTO  wanne  waliozaliwa na mama mmoja kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya wanaendelea vizuri.

Watoto hao walizaliwa na Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye amewashukuru wasamaria wema kwa kuendelea kuwapa misaada iliyosaidia watoto hao kukua vizuri.

Akizungumza na www.mbeyayetu.blogspot.com Nyumbani kwao jana Baba Mzazi wa watoto hao, Webson Simkanga(28) alisema yeye binafsi hana uwezo kiuchumi lakini kutokana misaada mbali mbali aipatayo kutoka kwa wasamaria wema inasaidia kuimarisha afya za watoto wake.

Alisema hivi sasa Watoto wake hao wamekua vizuri na kuleta matumaini kutokana na hali zao za kiafya na kuchangamka sana kinyume na matarajio ya watu wengi wasiokuwa na mapenzi mema kwa familia hiyo wakiombea mabaya kuwatokea.

Alisema kutokana na kuimarika kwa afya zao baba huyo ametoa majina kwa watoto wake hao huku akitarajia kuwabatiza kama ishara ya Wakristu ya kuwakabidhi watoto hao mikononi mwa Kanisa na Mungu.

Aliwataja majina watoto hao kuanzia wa kwanza hadi wa Mwisho kuwa ni Alinikumbu(mtoto mwenye huruma), Daudi, Asifiwe na Anania ambao anatarajia kuwabatiza Machi 9, Mwaka huu katika kanisa la African Mission Church(AMC).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Chiwanda, Ignas Sinkara, alisema jukumu la kijiji bado lipo palepale kuhakikisha hali za watoto zinaendelea kuimarika siku hadi siku na kuongeza kuwa pia Wasamaria wema wanazidi kujitokeza kuwachangia familia hiyo.

Alisema mbali na wanakijiji kujitokeza kwa wingi kumsaidia mama wanne kubeba watoto na kusaidia kazi za nyumbani taasisi zingine bado zinatoa misaada yao likiwemo Kanisa Katoliki ambalo lilichangia Fedha tyaslimu Shilingi 56,000/= pamoja na Debe mbili za Mahindi na kusaidia kuandaa shamba la kupanda Mihogo la Familia hiyo.

Aidha katika Ziara ya Waandishi wa habari Kijijini hapo yenye lengo la kutaka kuwajulia hali watoto hao ikiwa ni pmoja na kuwasilisha michango mbali mbali iliyotolewa na wasamaria wema kwa ajili ya familia hiyo.

Misaada hiyo ni pamoja na Msaada uliopokelewa ba Mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar Es Salaam wa www.michuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.

Msamaria mwema mwingine aliyejulikana kwa Norah SilverBoutique toka DSM ambaye ametoa Maziwa Lactogen Dazan Mbili yaani makopo 24 pamoja na nguo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Laki Tano.

Pia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini iliwezesha usafiri kwa wanahabari hao kwa kuchangia Mafuta, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hiyo Jijini Mbeya.

Na Mbeya yetu

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO