JESHI la polisi mkoani Arusha limeingia lawamani likituhumiwa kumuua
kwa kumpiga risasi daktari wa kitengo cha ukimwi katika hospitali ya
Selian,Japhet Mtingala alimaarufu Banda(48) mkazi wa Ekenywa wilayani
Arumeru kwa kumhusisha na tukio la ujambazi,ambapo watu wengine watatu
waliouawa wakidaiwa kupanga njama ya kupora fedha katika kituo cha
mafuta.
Picha YA mAKTABA na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
*******************************
Aidha inadaiwa kuwa,daktari huyo aliuawa wakati akipeleka dawa ya
kurefusha maisha ARV's kwa mgonjwa aliyekuwa katika bar ya Pama
iliyopo katikati ya jiji baada ya kukubaliana wakutane hapo.
Tukio la kuuawa kwa watu hao lilitokea Februali ,21 mwaka huu,majira
ya saa 1.30 usiku katika bar ya Pama iliyopo katikati ya jiji na
kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Liberatus Sabas
akidai ni majambazi waliokuwa wakipanga kwenda kupora.
Sabasi amewaeleza waandishi wa habari kuwa majambazi hao
walikuwawatano huku mmoja akifanikiwa kutoroka akiwa na silaha aina
ya SMG na kufanikiwa kupata silaha moja aina ya bastola ikiwa na
risasi kadhaa .
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu,Joel Samweli,amesema familia imejipanga
kushughulikia suala hilo,kupitia vyombo mbalimbali vya kisheria ili
haki ipatikane ,kwani alisisitiza mdogo wake hakuwa na chembe ya
ujambazi wa aina yoyote.
Akitoa salamu kwa niaba ya hospitali ya Selian,dkt David Mlaki
alieleza kusikitishwa na tukio hilo la kuuawa kwa muuguzi huyo na
kubainisha pasipo shaka kuwa marehemu hakuwa akijihusisha na matukio
ya ujambazi na kwamba wamepoteza maisha akitoa huduma ya dawa kwa
mgonjwa.
Mwili wa daktari huyo umezikwa na mamia ya wakazi wa maeneo
mbalimbalikatika shamba lake kijijini kwake na ameacha mke,aitwaye
Agnes Japhet,na watoto wanne ,ambao ni Felister ,Scolla,Justine na
Miriamu,huku mmoja wa watoto wake akisomeshwa kwa ufadhili wa
mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, mkaoni Arusha,Cyinthia
Mwilolezi.
Source: Nipashe
0 maoni:
Post a Comment