Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA Arusha Waunda Timu ya Uongozi wa Madiwani na Chama Kwa Utekelezaji Ahadi ya Kuwaletea Maendeleo Wananchi Kwa Ukaribu Zaidi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Kaskazini pamoja na Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Arusha mjini imekutana na madiwani wote wa Arusha Mjini kupitia chama hicho katika kikao maalumu kuunda umoja wa madiwani watokanao na CHADEMA kurahisisha utekelezaji wa ahadi za chama kwa wananchi.

Madiwani hao wamepewa semina  kupitia kwa Afisa wa Oganizesheni na Serikali za Mitaa Totinan Ndonde kuhusu masuala ya Serikali za Mitaa.

Sambamba na semina hiyo kumefanyika uchaguzi wa kuunda Umoja huo wa madiwani watokanao na CHADEMA kwa lengo la kurahisisha utaratibu wa kujisimamia. Kila ngazi itakua na vikao vyake na kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua kwasababu imeonekana kwasasa hawapati muda wa kukutana na kujadiliana.

Akifafanua zaidi Totinan ameeleza kuwa umoja huo utasaidia kuwaunganisha madiwani na viongozi wa chama ambapo kupitia mfumo huo kila ngazi ya uongozi na vikao vitahusisha viongozi wa chama na pia sehemu ya viongozi wa umoja huo watakua ni wajumbe wa Kamati Tendaji kwa ngazi husika.

Pamoja na hayo CHADEMA Kanda ya Kaskazini na Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Arusha Mjini walisimamia uchaguzi wa uundwaji wa umoja huo wa madiwani watokanao na CHADEMA kwa nafasi za  Mwenyekiti/Meya wa Halmashauri, Katibu, Mnadhimu, Mratibu na mawasiliano na Mtunza hazina.

Viongozi waliochaguliwa kuongoza umoja huo ni pamoja na
1. Isaya Doita  (Diwani wa Kata ya Ngarenaro) ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa umoja huo
2. Jeni L. Severe (Diwani wa viti maalum) ambaye amechaguliwa kuwa Katibu
3. Elirehema Nnko (Diwani wa  Kata ya Osunyai) amechaguliwa kuwa Mnadhimu
4. Ephata Nanyaro (Diwani wa Kata ya Levolosi) amechaguliwa kuwa Mratibu na mawasiliano na
5. Veronika H Malenge (Diwani viti maalum) amechaguliwa kuwa Mtunza Hazina.


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO