Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mashahidi watoa ushahidi wa kesi ya wizi na kutakatisha fedha inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa benki ya Exim benki tawi la Arusha


mahakama yakubali kupokea ripoti ya kichunguzi ya kesi ya exim bank

Shahidi wa 23 katika kesi ya wizi,kugushi na kutakatisha fedha zaidi
ya shilingi bilioni 7 inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa benki
ya Exim benki tawi la Arusha ,Mratibu Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la
polisi Makao Makuu,Crisantus Kitandala{44} jana alikabidhi ripoti ya
kiuchunguzi ya kimaandishi na vielelezo vyake juu ya wizi uliofanyika
katika benki hiyo.Kitandala ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Maabara ya uchunguzi wa
Kisanyansi wa Maandishi ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka
10 alisema kuwa ripoti hiyo imechunguzwa kwa kutumia mashine ya kisasa
ya video ya Comparator 6000 vsc 6000 na vifaa mbalimbali vyenye uwezo
wa kutambua miandiko mbalimbali inayobishaniwa.Shahidi huyo alisema hayo wakati akiongozwa na Mwanasheria wa serikali
Mwandamizi ,Poul Kaduchi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya
Wilaya ya Arusha,Deusdedict Kamugisha.Mtaalamu huyo wa maandishi wa Jeshi la Polisi alisema kuwa ofisi yake
ilipokea vielelezo vilivyokuwa vikibishaniwa vya benki nya Exim kutoka
ofisini ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai{RCO} Arusha novemba 24
mwaka huu.Shahidi huyo alisema katika uchunguzi wake wa unyambulishaji wa
kitaalamu na kisayansi wa miandiko   katika vitu vinavyobishaniwa vya
nyaraka za kibenki na miandiko ya baadhi ya watuhumiwa ilibainika
baadhi ya miandiko ilikuwa ikifanana na miandiko ya watuhumiwa wa kesi
hiyo.Alisema bahasha ya vielelezo vya benki ya Exim ilivyokuwa na
mihuri,risiti za kuweka na kutoa ,regista ya kuingia na kutoka
kazini,hundi za kuweka na kutoa na zenye saini ya baadhi ya watuhumiwa
,fomu mbali za kibenki zilizosainiwa na baadhi ya watuhumiwa zilikuwa
zikifanana na ripoti yake bila ya kuwa na shaka yoyote katika
uchunguzi wake.Mtaalamu huyo alisema RCO Arusha alikuwa akitaka uchunguzi ufanyike
kulinganisha saini na maandishi na alama za mihuri zilizokuwa
zikibishaniwa na aligunduwa kuwa baadhi ya saini na miandiko ilikuwa
sahihi kwakwa baadhi ya watuhumiwa.Shahidi aliwataja baadhi ya watuhumiwa kuwa ni pamoja na Mosses
Chacha,Liliani Mgeye,Tutufye Mwakipesile ,Neema Kinabo ,Pamphir Lubuva
,Deusdedict Chacha na Shijana Matumbo na wengine miandiko yao ilikuwa
ikifanana na uchunguzi aliofanya.‘’Uchunguzi wangu ulikamilika januari 27 mwaka huu na ripoti ya
uchunguzi huo niliipeleka ofisi ya RCO Arusha siku hiyo hiyo na nakala
ya uchunguzi alikabidhiwa Kamishina kwa niaba ya Mkurugenzi wa kitengo
hicho’’alisema KitandalaAwali kulizuka malumbano ya kisheria kati ya mawakili wa watuhumiwa
ambao walipinga ripoti hiyo kupokelewa na mahakama  kama ushahidi kwa
maelezo kuwa ilikuwa na kasoro mbalimbali za kisheria na mhusika
hakupaswa kuitoa yeye mahakamani hapo.Hata hivyo Hakimu Kamugisha alitupilia mbali pingamizi hilo na
kumwamuru shahidi kutoa taarifa hizo mahakamani hapo kama ushahidi
kwani yeye ndiye mhusika mkuu wa ripoti hiyo.Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa tena leo wakati shahidi
huyo akiendelea kutoa ushahidi wake kwa siku ya tatu mfululizo katika
mahakama hiyo.Watuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa meneja wa benki
tawi la Exim Arusha Bimel Gondalia{37},Lilian Mgaya{33} mshitakiwa wa
tatu Neema Kinabo{30}ameachiwa baada ya kukiri kosa na kulipa fainina
mshitakiwa na nne ni Livistone Julius{36}.Wengine ni pamoja na mshitakiwa wa tano Joyce Kimaro{36},mshitakiwa wa
sita ni Daud Mosha,mshitakiwa wa saba ni Doroth Tigana{50} Evans
Kashebo{40},mshitakiwa na tisa Mosses Chacha{37}ameachiwa baada ya
kukiri kosa na kulipa faini ya shilingi milioni 100 mshitakiwa wa kumi
katika kesi hiyo Tuntufe Agrey{32}.Mshitakiwa wa kumi na moja katika kesi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya
watu wa Jiji la Arusha ni Joseph Meck{34},Janes Massawe{32} mshitakiwa
wa kumi na mbili,mshitakiwa wa kumi na tatu ni Christopher Lyimo{34}na
mfanyabishara wa Arusha Gervas Hugo ambaye ni mshitakiwa wa kumi na
nne.

Washitakiwa wanne tu ambao ni Gomes mshitakiwa wa kwanza,mshitakiwa wa
nane Kashebo,mshitakiwa wa kumi na moja Meck na Lyimo wako nje kwa
dhamana kwani hawakushitakiwa na shitaka la utakatishaji fedha  lakini
washitakiwa wengine wote wako rumande kwa makosa ya utakatishaji fedha
haramu kwani kesi hiyo haina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Mwisho
Inbox
x

vero ignatus <ignatus66@gmail.com>

1:29 PM (4 hours ago)


to Obed, hussein, Isaac, Eliphace, jmungaya, johnnygagarini
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO