Na Ferdinand Shayo,Arusha .
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amewatunuku zaidi ya wahitimu 50 waliohitimu katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji (AJTC) huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za jamii na kuleta mabadiliko kupitia kalamu zao.
Kalisti amewataka Wanahabari kujikita katika kuandika habari za kijamii zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuleta suluhu kwenye matatizo ya jamii.
Ameishauri serikali kuangalia upya mswada wa habari na kuufanyia marekebisho katika vipengelea ambavyo vinaminya haki ya habari.
Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ,Joseph Mayagila amesema kuwa tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi kwani bila taarifa hakuna maendeleo.
Alisema kuwa ni vyema serikali ikatazama upya utekelezaji wa sheria mpya na kufanyia kazi mapungufu ili wanahabari waendelee kuwahabarisha Watanzania
Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) wakirusha kofia juu ishara ya kuonyesha kutunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada |
0 maoni:
Post a Comment