Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAZIRI MPANGO AHOJI CHANGAMOTO ZINAZOZIFANYA TAASISI HIZI ZA KIFEDHA KUTOIKOPESHA SEKTA YA KILIMO






Image result for PHILIP MPANGO WAZIRI
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Gavana wa Benki Kuu nchini Tanzania Benno Ndulu
Wa kwanza kuilia ni Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango  ni Gavana wa Benki kuu nchini Tanzania Benno Ndulu wakibadilishana mawazo.






Wa kwanza kuilia ni Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango  ni Gavana wa Benki kuu nchini Tanzania Benno Ndulu wakibadilishana mawazo.
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango  na Gavana wa Benki kuu nchini TanzaniaBenno Ndulu wakisalimiana.
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo chakimataifa cha mikutano AICC leo jijini Arusha.
Sekretaireti ya Taasisi ya fedha wakiwa katika picha ya pamoja  wa tano kutoka kulia niNaibu  Katibu mkuu Wizara ya fedha na mipango Amina Shabaan,wa tano kuitoka kushoto ni Waziri wa fedha na mipango ,aliyepo kulia kwake ni Gavana wa Benki kuu nchi Tanzania Benno Ndulu.

Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za fedha wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa fedha na mipango Dkt. Philip Mpango katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC mkoani Arusha.


Na.Vero Ignatus Arusha.

Mkutano wa 18 wa  ulioandaliwa na Benki  kuu  ya Tanzania ambayo imezishirikisha taasisi zote  za kifedha ,mabenki,taasisi za mifuko ya jamii ,umezinduliwa  rasmi leo mkoani Arusha na waziri wa fedha na Mipango , Dkt  Philip Mpango


Mkutano huo ambapo unafanyika kila baada ya miaka miwili umezinduliwa leo katika kituo cha mikutano cha kimataifa Aicc unafanyika ukumbi wa simba ukiwa na dhamna ya kukaa kwa pamoja kuzungumzia ni nanma gani Tanzania inapaswa kutumia  fursa yake ya kigeografia ili kuweza kuendeleza taifa.


“ Fursa hizi ni nyingi ukizingatia nchi ya Tanzania ipo katikati ya bara la Afrika  imenaopakana na  upande wa bahari  ya hindi ,hivyo nchi hii inayonafasi kubwa sana kibiashara ya meli kutoka mashariki ya mbali China Uarabuni Afrika kusini na Afrika ya kaskazini nchi hii twaweza kutumia fursa hii kuendeleza fursa hii ya viwanda ambayo ndiyo dhamira kuu ya serikali hii ya awamu ya tano.”amesema Mpango.


Tanzania tunarasilimali nzuri  ikiwemo madi ya kila aina  kuna maswali nimewauliza maswali ambayo ningependa wataalamu wa fedha wajiulize:

 (1(2)wamejipangaje kuwasaidia taasisi na  makampuni madogowadogo ili waweze kupata mtaji (3)sekta ya kilimo ndipo watanzania wengi walipo 
wanasaidiaje sekta hii ya kilimo ili waweze kutumia ardhi hii nzuri ili tuweze kujenga uchumi wetu ukizingatia tuna vijana wenyenguvu ukizingatia ndiyo muhimili mkubwa wa uchumi wetu.
(4)Nichangamoto gani zinafanya taasisi hiziza fedhya hazikopeshi sekta za kilimo?

Amezitakaa taasisi za fedha  zenyewe zitoke  ziende hadi vijijini  nkuwaelezea  wananchi  fursa ambazo zipo  za kuwapatia wananchi mikopo  ya kuendeleza shughuli zao binafsi  ili waweze kujikwamua kiuchumi  pia amewataka watumie vyombo vya kisasa kutoa elimu kwa wananchi ili wananchi waelewe taasisi hizi za fedha wanaomlango wa kuwapatia mitaji ya kuendeleza shughuli zao.

Kwa upande wa Gavana wa benki kuu nchini Tanzania Benno Nduluamesema kuwa  kwa upande wa sekta ya fedha  kitu kikubwa ni kuwaasa mabeki na taasisi za fedha kuhakikisha kuwa wamewafikia watanzania katika kuweza kuwashirikisha mchango wa kifedha amesema kwa kila sh 40% katika 60% ndiyo wanayo wao kama benki, amesema kuwa ili kuipata hiyo 60% ni kwa kupitia mitandao mingine ya kifedha ya simu kwani  Sitini ipo nje ya mfumo wa kifedha .

Amesema mabenki yanaweza kutoa mkopo wenye masharti  nafuu kusudi la kufanya hivi ili na wao waweze kutafuta fedha za kudumu na siyo zile za kuingiza siku moja na kutoka,amesema katika kikao kilichopita walikubaliana namna ya kuwakopesha wakulima lakini inaonekana kuwa unapokopesha lazima urudisha katika sekta ambayo fedha hazirudishwi ni sekta ya kilimo ,hata kama una pesa unaogopa kumkopesha fulani na lazima kuangalia kama taarifa za mkopaji zipo sahihi.

"Katika sekta ambayo ni ngumu kuikopesha ni sekta ya kilimo pesa hazirudi,na hata kama unafedha unaogopa kumkopesha mtu ambaye harudishi ,ndiyo maana tunaangalia tutakapomaliza kikao chetu hiki cha siku mbili tuytakuwa tumepata muafaka tufanyeje katika sekta hii ya kilimo."alisema Gavana Benno.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO