Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani( RSA)aliyeshika kipazasauti pichani Stella Rutaguza ,akitoa ufafanuazi kwa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro majukumu ya kiutendaji ya RSA .Wakwanza kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charlers Mkumbo,waliovaa tshirt nyeupe ni mabalozi wa usalama barabarani mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog. |
Mabalozi wa
usalama barabarani mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya kushiriki katika wiki ya nenda kwa usalama iliyozinduliwa hivi
karibuni mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Makamu
mwenyekiti wa RSA mkoa wa Arusha akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arusha
mjini Gabriel Daqqaro kipeperushi chenye maelezo mbalimbali kuhusu(
RSA)Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa
wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akiweka saini kwenye
kitabu cha wageni alipotembelea banda la (RSA)Katika wiki ya nenda kwa
usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni katika uwanja wa mpira
wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusa.Picha na Vero Ignatus
Blog.
Mwenyekiti wa (RSA)Mkoa wa Arusha Stella Rutaguza
akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqqaro
alipowasili katika uwanja wa Shekh Amri Abeid ,ambaye alimuwakilisha
mkuu wa mkoa wa Arusha katika wiki ya nenda kwa usalama na kupokelewa
na kamati ya maandalizi ya mkoa ya usalama
barabarani.
Balozi
Vero Ignatus akisalimiana na mkuu wa wilaya mkuu wa wilaya ya Arusha
Mjini Gabriel Daqqaro ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa
Arusha alipowasili katika uwanja wa Shekh Amri
Abeid na kupokelewa na kamati ya maandalizi ya mkoa ya usalama
barabarani.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na Vero
Ignatus Arusha.
Operesheni
abiria
paza sauti inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika mkoani Arusha ikiwa na
lengo la kumuelimisha abiria pamoja wanawatumiaji wa vyombo vya moto kuwa
makini kutii na kufuata sheria za usalama barabarani .
Hayo
yamesema na mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Stella Rutaguza
alipokuwa kwenye wiki ya nenda kwa usalama iliyozinduliwa hivi karibuni mkoni
Arusha amabapo kilele chake kilikuwa tar 11novemba katika uwanja wa mpira
Shekh Amri Abed jijini Arusha.
Stella
amesema kuwa abiria anatakiwa kufunga mkanda akiwa ndani ya chombo cha
usafiri,kuripoti
vitendo vyote vinavyohatarisha usalama wa abiriaikiwemo mwendo kasi,ulevi wa
dereva,upitaji wa hatari wa magari mengine bila kufuata sheria na alama za
barabarani,dereva kuzun gumza na simu akiwa anaendesha,pamoja na lugha chafu ya
uhasama kwa abiria.
Bi
Rutaguza amesema kuwa jukumu la kuzifanya barabara zetu kuwa salama ni la kila
mtu ,hivyo kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake,tusiwaachie askari wa
usalama barabarani peke yao kwani hawawezi kuwa kila mahali.
“Suala la
usalama barabarani ni la kila mtu ,maana usipotumia usafiri binafsi utatumia
usafiri wa jumuia,au hata pikipiki ilimradi umesafiri ndiyo maana kila mmoja
anatakiwa awe mlinzi wa mwenzie ,kwa kutoa taarifa pale unapoona dereva anakiuka
sheria ya usalama barabarani ili tuweze kuepuka ajali zinazosababishwa na
uzembe pamoja na ulemavu”alisisitiza Bi Stella.
Amesema
kuwa operesheni paza sauti inafanyika kwa miezi mitatu ikiwa na lengo la
kuelimisha ,kukemea,na kutoa ripoti kwa jeshi la polisi kitengo cha isalama
barabarani,abiria kufahamu haki yake awapo ndani ya chombo cha usafiri,hatakiwi
kukaa kimya aonapo dereva anavunja sheria za usalama barabarani.
Ameainisha
haki za abiria kwa mujibu wa kanuni za usafirishaji za Sumatra,abiria
kurudishiwa nauli chombo kinapochelewa kuanza safari ndani ya saa mbili au
chombo kuharibika,kupewa tiketi ndani ya ofisi,kutonyanyaswa kwa lugha ya
matusi,abiria kufikishwa mwisho wa safari,kulipa nauli iliyoidhinishwa
na Sumatra
na nyingine nyingi.
Amewataka
abiria wasikubali kuchanganywa kwenye vyombo vya usafiri pamoja na
wanyama,au mizigo ya hatari ndani ya gari kama vile misumari,gesi, na
milipuko, amesema abiria anatakiwa afahamu kuwa yeye siyo mateka wa
dereva bali ana haki ya kusafiri salama kutokana na nauli
aliyolipa,ambayo ni mkataba kati yake na mwenye gari na siyo
upendeleo.
0 maoni:
Post a Comment