Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania Mathias Canal akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness
Lwiza baadhi ya mahitaji kwa ajili ya wazee waishio kituoni hapo.
Kushoto ni Mkurugenzi
wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining
and Environmental Transformation for Development Organization) Bw Ashraf Omary akimsikiliza kwa makini mzee aliyelala kutokana na homa kali inayomsumbua
Kushoto ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya
Ibosa akisisitiza jambo kwa Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni katibu wa TAWSO Mwanza Bi Abigali Mhingo
Meneja Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein Sungura akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya uongozi wa METDO Tanzania katika kituo cha Wazee KIILIMA Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera
Hiki ndicho Choo kinachotumiwa na wazee waishio kambi ya KIILIMA-Bukoba
Moja ya Mzee katika Kituo cha Wazee KIILIMA akiwa amelala kutokana na homa kali iliyokuwa inamsumbua
Mahitaji yamepokelewa kwa furaha na wazee wote kupitia uongozi wao
Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu,
Kushoto kwake ni Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali
ya METDO Tanzania, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Ndg Charles
Mafimbo, Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Hussein Sungura Meneja Mradi METDO
Tanzania na Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ndg Ashrafu Omary
Mkurugenzi
wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining
and Environmental Transformation for Development Organization) Bw Ashraf Omary akifanya usafi katika jiko la watumishi wa kituo cha wazee KIILIMA
Mjadala ukiendelea baada ya kazi kumalizika Kijijini KIILIMA kambi ya wazee
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza akipanda mti kwa ajili ya kumbukumbu
Tafakuri pana kwa Mzee Wilson Ziraimanikabla ya kukabidhiwa mahitaji na uongozi wa METDO Tanzania
Nyumba ya kulala wazee wa kituo cha KIILIMA kilichopo Kata ya Nyakato Mkoani Kagera
Viongozi wkibadilishana mawazo mara baada ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA
Kijana ni mzee ajaye na Mzee ni kijana aliyekuwa
Hili ndilo jiko linalotumiwa na viongozi wa kituo cha KIILIMA kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba
Katikati ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya
Ibosa akipata maelezo ya awali kwa Moja ya mzee aishie kambini KIILIMA kabla ya kumfanyia vipimo
Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania akipanda mti wa matunda aina ya Mlimao kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA
Majadiliano ya namna ya kuchimba mashimo kabla kupanda miti
Moja ya nyumba anayoishi Mtumishi wa Kituo cha wazee KIILIMA Kilichopo Mkoani Kagera
Mkurugenzi wa METDO Tanzania Bw Ashraf Omary mwenye Jembe akimsaidia kazi Mzee Wilson Ziraimani, Mzee huyu
alikuwa anafanya kazi za kilimo katika mashamba mbalimbali nchini, yeye
ni mkazi wa Ngara na wakati akiwa mtoto alikuwa analelewa na Mama wa
kambo.
Aliwasili katika kituo cha kulelea Wazee cha KIILIMA Mwaka
1986 hapo alipo anatambaa kwani alivunjika kiuno enzi za ujana wake
baada ya kuanguka mtini wakati alipokuwa anakata kuni kwa ajili kupikia.
Viongozi wa METDO Tanzania, Kiongozi wa TASWO, na Viongozi wa kituo cha Wazee KIILIMA wakipanda mti wa matunda aina ya Parachichi kwa ajili ya kumbukumbu na kampeni ya upandaji miti
Na
Mathias Canal, Bukoba
Kukosekana kwa huduma bora na msingi kwa
wazee nchini imetajwa kuwa changamoto kubwa kwa Wazee waishio katika kambi mbalimbali
za serikali na zile za binafsi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Asasi
isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and
Environmental Transformation for Development Organization) Bw Ashraf Omary wakati akikabidhi mahitaji kwa wazee wa kituo cha
KIILIMA kilichopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Bw Omary alisema
kuwa Asasi hiyo yenye usajili No. ooNGO/08317 inajishughulisha na kutoa Elimu
ya Mazingira kwa wananchi wanozunguka migodi pamoja na wafanyakazi wa migodini
ambapo pia imejikita kuwasaidia wazee waishio katika kambi mbalimbali nchini
katika huduma za kuwapatia mahitaji ya msingi ya kila siku kama vile (Chakula,
na Mavazi) sambamba na kutoa huduma ya upimaji wa afya zao kupitia wataalamu wa
tiba na kuwapatia dawa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali.
Alisema kuwa
kumekuwa na wimbi kubwa la wazee kutopatiwa huduma bora ikiwemo chakula na
matibabu jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia wazee wengi kufariki pasina
huduma yoyote ya kitabibu sambamba na kukosa Lishe Bora.
Bw Omary ameushukuru
uongozi wa kampuni ya ZONGII PUMBLING
LTD ya Jijini Mwanza kwa kushirikiana na METDO Tanzania kufanikisha kupatikana
mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wazee wa kambi ya KIILIMA sambamba na
kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa ushirikiano ulioonyesha ikiwa ni
pamoja na kuruhusu madaktari kwa ajili ya kwenda kuwapima afya wazee hao.
Kwa upande wake Meneja
Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein
Sungura amebainisha kadhia zinazowakumba wazee katika kituo cha KIILIMA
sambamba na vituo vingine nchini kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za usafiri
ili kurahisisha wazee kufikishwa haraka hospitalini pindi wauguapo, Ufinyu wa
Bajeti, Ukosefu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya usafi na ucheleweshaji wa
Ruzuku ya serikali.
Sungura alisema
kuwa Mpaka sasa Asasi hii ya METDO Tanzania imesaidia katika maeneo mbalimbali
ikiwemo tukio la Agosti 13, 2016 la kumuenzi Mwl Julius Kambarage Nyerere
katika Makao ya wazee wasiojiweza BUKUMBI Mwanza, Tukio la Octoba Mosi 2016
SIKU YA WAZEE DUNIANI katika wilaya ya Shinyanga ambapo jamii ilishirikishwa kutambua
changamoto zilizopo katika kituo cha Wakoma na Wazee wasiojiweza cha KOLANDOTO pamoja
na Kituo cha Wakoma na Wazee wasiojiweza
cha NYABANGE BUTIAMA na kuwa sehemu ya
kuzitatua changamoto hizo.
Kutokana na kazi
hiyo ya wito inayofanywa na METDO Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali
Salim Kijuu ametoa wito kwa Asasi hiyo kuwekeza Mkoani Kagera katika sekta
mbalimbali ikiwemo kilimo ili ushirikiano wa kusaidia wazee uweze kukomaa na
kusaidia wazee wote nchini kirahisi sambamba na kutoa fursa kwa vijana kutambua
umuhimu wa kufanya kazi sawia na kujiajiri.
Kijuu alisema kuwa
kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na hali nzuri ya hewa na udongo wake kuwa na
rutuba ni vyema Asasi ya METDO Tanzania ikafanya kazi yake kwa misingi ya
katiba lakini pia inapaswa kuwasaidia vijana wengi nchini ili kuachana na uvivu
walionao badala yake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika
kuisimamia na kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.
Akisoma taarifa ya
kituo hicho Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza alisema kuwa Kituo hicho kina jumla ya wahudumiwa
24 ambapo kati yao kuna watoto 6 waliokuwa kwenye mazingira hatarishi baada ya
kutelekezwa na wazazi wao huku wengine wakipokelewa baada ya wazazi wao kufariki
kutokana na janga la UKIMWI lililotokea mwaka 1984.
Hata hivyo amewaomba
wadau mbalimbali kujitokeza na kuwachukua watoto hao kwani kuendelea kubaki
katika kituo hicho sio jambo jema kwao kwani wanachanganyikana na wazee ambao
wengi wao wana matatizo ya akili.
Lwiza amesema kuwa
kufuatia uharibifu wa majengo kutokana na Tetemeko lililotokea hivi karibuni Mkoani
Kagera na kuharibu majengo mengi kituoni hapo imesababisha kukosekana kwa
nyumba za watumishi, na choo kwa ajili ya matumizi ya wazee pamoja na watumishi
wa kituo hicho.
Naye Dkt Peter
Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa ameiomba serikali kusaidia
upatikanaji wa sehemu maalumu ya kuhifadhia dawa, kutolewa mafunzo ya tiba kwa
wahudumu waliopo kituoni hapo sambamba na kupatikana kwa vifaa tiba kwa ajili
ya kupima damu, Sukari, MRTD, Presha na wingi wa damu.
Kituo cha Wazee
KIILIMA kilichopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kilicho chini ya Wizara ya
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni moja kati ya vituo vya
kulelea wazee hapa nchini ambapo awali kilikuwa chini ya kanisa la Roman Catholic
na baadaye kilikabidhiwa rasmi kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mnamo mwaka 1974.
Baada ya
kutembelea vituo vyote vya Wazee kanda ya Ziwa METDO Tanzania inataraji kuzuru
Mikoa ya Kanda ya kati kwa ajili ya kujionea changamoto za wazee mbalimbali
waishio kambini na kuzifikisha sehemu husika wakiwemo viongozi wa dini, Wafanyabiashara,
Serikali na Wadau mbalimbali nchini.
0 maoni:
Post a Comment