Serikali inajipanga kwajili wataalamu wa maendeleo ya jamii 5,554 kwa kipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya Serikali kuu hadi kijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu ya kwanza nchini.
Ameyasema hayo katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji la Arusha Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla amesema serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata.
Aliongeza kuwa kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii wameanza kupungua sana na kukitaka chuo kuongeza udaili wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu awa kila wilaya na kata.
Aidha aliitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa taaluma yenye viwango na bora na uzingatiwe katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu
CHANZO: VERO IGNATUS
0 maoni:
Post a Comment