Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA GESI NA MAFUTA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wataalamu wa masuala ya gesi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wazalishaji Petroli Afrika, Mhandisi Mahaman Laouan Gaya mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha rasilimali ya gesi na mafuta inakuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa taifa na wa wananchi kwa ujumla.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo 22-Nov-2016 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya gesi na mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya Getenergy ya Uingereza.
Katika hotuba yake, Makamu wa Rais amewahakikishia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi na itakuwa bega kwa bega na wadau wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha uwekezaji utakaofanyika unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
Amesisitiza kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inaendelea na mkakati kabambe wa kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao ambao watakuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa katika sekta za gesi na mafuta.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na ana imani kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana hivyo ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kujipanga kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha watakaoshikiri katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanajihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa rasilimali ya gesi na mafuta zitakagundulika na kuchimbwa barani Afrika zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo, uchumi ambao utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi katika nchi husika.
Mkutano huo wa siku Mbili wa Kimataifa umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia bora za uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.
Kwa upande wake,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kwa Serikali itaendelea kusomesha wataalamu wake ndani na nje ya nchi ili kujitosheleza kwa wataalamu wa sekta hiyo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO