Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MBUNGE LEMA AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, ARUDISHWA MAGEREZA

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema amekwama kwa mara ya tatu hii leo kupatiwa dhamana kufuatia kushikatikwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa makosa ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.

Mahakama Kuu kanda ya Arusha imetupilia mbali maombi ya Lema kupitia mawakili wake kuitaka Mahakama hiyo kufanya rejea ya Hukumu ya Mahakam ya Hakimu Mkazi iliyomnyima dhamana badala ya kutoa mashartiya dhamana kama ambavyo ilikuwa imeamua awali.

Mbunge huyo alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma Novemba 3, 2016 ambapo alishikiliwa kwa muda katikaKituo Kikuu cha Polisi Arusha, kabla ya kufikishwa Mahakamani kwa Ombi la Mawakili wake Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Mmoja wa mawakiliwanaomtetea Lema, John Mallya ametoa taarifa ifuatayo kuhusiana na kilichoamuliwa hii leo "Mahakama Kuu haijamnyima Lema dhamana, ilichoamua leo ni kuwa Lema anayo haki ya kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu dhidi ya maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya kusema amefungwa mikono na notisi ya rufaa iliyotolewa na upande wa Jamuhuri ikiwa tayari alishapewa dhamana na anasuburia masharti ya dhamana.

Mawakili wa Lema tupo Mahakama Kuu Arusha wakati huu na tutawasilisha rufaa hiyo leo.
Anabaki rumande sio kwasababu Mahakama Kuu imemnyima dhamana bali anasubiri siku Mahakama  Kuu itakapotengua maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi.
John Mallya
22/11/2016"
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa nje ya Ukumbi wa Mahakama Kuu hii leo baada ya mahakama kuwaelekeza kukata rufaa badala ya kuiomba kufanya rejea.


Baadhi ya MwakiliwaMh Lema, kutoka kushoto Peter Kibatala, Sheck Mfinanga na James LyatuuWashirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO