Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

LOWASSA, WABUNGE NA VIONGOZI WENGINE CHADEMA WAKO NA ZIARA YA KIMYAKIMYA NCHI NZIMA KUIMARISHA CHAMA

Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Mh Edward Lowassa akilakiwa na wananchamawenzake mjini Dodoma alipowasilikwa vikaovya mabaraza ya chama hicho kwamikoa ya kanda ya kati leo.

Mh Lowassa katikakikaocha ndani Mjini Dodoma kukaguauhai wa mabaraza ya CHADEMA leo.

Siku ya jana,CHADEMA walitoa taarifa ifuatayo ikieleza kwa undani ziara hizo za kimyakimya za viongozi wakuu wa CHADEMA. 


Viongozi Waandamizi wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe leo wameendelea na ziara ya kikazi inayohusisha vikao vya ndani katika majimbo ya Kanda ya Kati (Dodoma, Morogoro na Singida), ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama kwa kanda hiyo utakaofanyika Novemba 23, mwaka huu.
Mwenyekiti Mbowe anaongoza timu inayokwenda katika majimbo ya Mkoa wa Morogoro, akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu Prof. Mwesiga Baregu, ambapo jana walikuwa majimbo ya Mlimba na Kilombero na leo wamefika majimbo ya Mikumi na Kilosa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Tanganyika), Prof. Abdalla Jumbe Safari anaongoza timu iliyoko mkoani Dodoma, akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim, jana walifika majimbo ya Kongwa na Mpwapwa na leo wamefanya ziara katika majimbo ya Chemba na Kondoa Kaskazini na Kondoa Kusini.
Timu ya tatu inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambapo jana walikuwa katika majimbo ya Singida Mashariki, Singida Magharibi, Singida Mjini na Singida Kaskazini na leo wamefika majimbo ya Manyoni Mashariki na Manyoni Magharibi (Singida) na Bahi (Dodoma).
Katika ziara hiyo, Viongozi Wakuu pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu wameambatana na wabunge ambao wamegawanywa katika timu mbalimbali na kupangiwa majukumu kwenye kanda 8 za upande wa Tanganyika, kati ya Kanda 10 za chama nchi nzima.
Siku ya Jumanne, Novemba 22, timu zote zitaendelea na ziara katika majimbo mengine katika mikoa hiyo mitatu kadri ya ratiba ya ziara nzima ilivyopangwa.
Novemba 23, mwaka huu Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Kanda ya Kati watakutana kwa ajili ya kikao cha uchaguzi, kuchagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mweka Hazina wa Kanda.
Imetolewa leo Jumatatu, Novemba 21, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA


Mh Lowassa akipokelewa na viongozi wa CHADEMA na wananchi Wilayani Kongwa janaWashirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO