Rufaa ya Dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema anayeendelea kusota rumande kwa dhamana yake kuzuiwa na Serikali kutokana na mashitaka ya kutoa maneno ya uchochezi kwa Rais Magufuli imepangwa kusikilizwa siku ya tarehe 28/11/2016 mbele ya Jaji Mwandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Jaji Fatma Masengi.
Maombi hayo ya rufaa namba 112/113 yalisajiliwa katika Mahakama hiyo jana Novemba 23, 2016 na Mawakili kutoka TANAFRICA LAW wakiongoozwa na Wakili Peter Kibatala kutokana na makosa ya kisheria yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Awali mawakilihao na mteja wao walipwa maelekezo na Mahakama Kuu walikolalamika na kuomba marejeo ya hukumu ya Hakimu Mkazi wakidai Hakimu Desdery Kamugisha alikosea kisheria kuruhusu rufaa ya mawakili wa serikali kuweka zuio la dhamana ilhali alisharuhusu dhamana kwa mshitakiwa na kwamba ni masharti ya dhamana tu ndio yaliyokuwa ynasubiriwa.

Picha ya Makataba: Lema na wafuasi wake wakitoka katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha wakati akifuatilia kesi yake ya Ubunge miaka ya nyuma |
0 maoni:
Post a Comment