Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UFAHAMU MMEA HATARI WA GUGU KAROTI NA MADHARA YAKE


Kutoka kushoto ni  Beatrice John mmoja wa wafanyakazi waChuo kikuu cha  Mount meru akifuatiwa na aliye kushoto kwake Afisa uhusiano wa Chuo hicho bi Imelda Naomi wakiwa wameshikilia mmea wa gugu karoti baada ya kuling'oa wakiwa wamevaa mifuko ya plastiki.


Wafanyakazi wa chuo kikuu cha Mount Meru Philipo Meleji na Boniface Msuta , wakiwa wameshikilia mmea hatari wa gugu karoti baada ya kuung'oa wakiwa wamevaa mifuko ya plastiki ili kuzuia majani yake yasigusane na ngozi ya mwili.
Ndugu Gaston Baruan mmoja wa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Mountmeru akiwa ameshika gugu karoti kwa mfuko wa plastiki akiwa ameling'oa tayari.
Mmea hatari wa gugu Karoti ukiwa umeota pembezoni kwa nyumba .Picha kwa idhini ya chuo kikuu Mount Meru.

Na.Vero Ignatus,Arusha.
Baada ya kupata elimu juu ya mmea hatari wa gugu karoti ambao una madhara kwa afya ya binadamu ,wanyama na mimea ,waalimu ,wafanyakazi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mount Meru wameungana kwa pamoja kung'oa mmea huo katika maeneo yao na kuuteketeza kwa moto.
 
Wafanyakazi hao walipate elimu kuhusiana na mmea huo hatari  kutoka kwa wataalam wa kituo kinachohusika na teknilojia za Kilimo na mifugo  (ECHO) kilichopo Ngaramtoni Mkoani Arusha.

Mmea huo hatari wa gugu karoti ni hatari kwa afya ya binadamu,wanyama na mmea mingine,ambapo kwa mwanadamu mmea huo unasababisha harara katika ngozi,na kuharibu mfumo njia ya hewa (husababisha pumu)

Aidha  mtaalam huyo Charles Bonaventure amesema kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa wafugaji kuwa ng'ombe wao wamekufa baada ya kula mmea huo
Amesema kuwa ng'ombe waliokula mmea huo maziwa  yanakuwa machungu .

Mtaalam huyo amesema kuwa kutokana na utafiti uliokwisha kufanyika inaonyesha kuwa ng'ombe akila kwa 10% hadi 50% mfululizo huweza kufa

Aidha wanaiomba serikali hususani wizara ya Kilimo mifugo na uvuvi,wizara ya Afya,maendeleo ya jamii  wazee na watoto, wadau mbalimbali  wa mazingira,kuangalia namna gani wanaweza kuutokomeza mmea huo ambao umezagaa katika mkoa wa Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Kagera

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Chuo Kikuu cha Mount Meru bi Imelda Naomi amesema kuwa wamefarijika kupata elimu juu ya mmea huo hatari kwani mara zote wamekuwa wakiuona mmea huo bila kufahamu madhara yake

Amesema kuwa elimu hiyo waliyoipata watashirikiana kuitoa kwa wengine ili waweze kuelewa madhara ya mmea huu hatari wa gugu karoti ili wasiweze kupata madhara

Aidha wameiomba serikali kuingilia kati swala la mmea huo kwani linaenea kwa kasi kubwa mno.

CREDIT: VERO IGNATUS
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO