RAS TANGA ATAKA WAANDISHI WA HABARI KUPEWA USHIRIKIANO
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo |
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Msaidizi Alex Abraham |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Amina Omari naye akipokea cheti hicho |
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na Mwandishi wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea cheti |
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea cheti |
Mmiliki wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga,Salum Mohamed naye akipokea cheti hicho |
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo
akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo |
Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani Tanga,Frank Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo leo |
Sehemu ya waandishi wa habari
mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo
Sehemu ya waandishi wa
habari mkoani Tanga
wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki
wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF),Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwandishi wa gazeti la Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Klabu)Neema Omary kulia na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo,Amina Omari wakifuatilia matukio
mbalimbai
KATIBU Tawala Mkoa Tanga
Mhandisi Zena Said ameziagiza
taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa
habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye taasisi hizo kwa ajili ya
kuhabarisha umma.
Ameyazungumza hayo leo wakati
wa kuadhimisha siku ya
uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa Tanga maazimisho hayo
yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za
kiserikali.
Hatua hiyo imekuja mara baada
ya waandishi wa habari kutoa
malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi
katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya taasisi za Serikali kushindwa
kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji kutekeleza majuku
yao ya kazi.
Burhan Yakubu ambae ni mjumbe
na mwaandishi wa habari alisema kumekuwepo na
utaratibu usioendana na
maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza
urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi
anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali
hiyo
“Tumekuwa tukikwama kutekeleza
wajibu wetu hasa tunapohitaji
kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali
kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo limekuwa liktkwamisha katika shughuli
zetu”Alisema Yakubu.
Akitolea ufafanuzi malalamiko
hayo Mhandisi Zena alisema taasisi zote zinapaswa
kutambua kuwa
wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii
na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza
majukumu yao.
Mhandisi Zena alisema
zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa
waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa
ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka kutekeleza
wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Tusiwawekee mipaka waandishi
wakati wanapotaka kutekeleza
majuku yao na tayari nimekwisha toa agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa
taasisi zote,hakuna jambo linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata
kwa wakati ikiwa hakuna waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni
kubwa kwa Taifa Hili.”Alisema
Hata hivyo alitumia fursa hiyo
kuwaomba waandishi wa habari
kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili yatakayokuwa na maslahi mapana kwa
ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa
kwenye machafuko.
Katika hatua nyingine Mwandishi
wa Tanzania Daima Mkoani
Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi
Mkoa Tanga,Kamishna Msaidiz,Mwandamizi wa Polisi Benedict Wakulyamba,juu ya
usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano
ya kisiasa.
Mbaruku alisema hivi karibuni
kumeripotiwa kutokea matukio
kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali hapa nchini kufanyiwa
vitendo vya udhalilishaji na kushindwa kuwajibika katika harakati zao za kupata
habari kwa lengo la kuhabarisha umma na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu
ya usala wa maisha yao.
Kamanda wakulya alisema jukumu
la usalama lipo mikononi mwa
jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua uwepo wa waandishi na umuhimu wao
katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa waandishi hao kuziona dalili za
uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema kabla ya madhara makubwa hayaja
tokea.
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha.
0 maoni:
Post a Comment