Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TADB YAOMBWA KUSAIDIA SEKTA YA MIFUGO MKOANI ARUSHA

Wadau wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa.
Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, kwa niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.

Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga. 

Naye, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Mkoa wa Arusha unashika nafasi ya tatu kati ya mikoa yenye mifugo mingi nchini ambapo inakadiriwa kuwa na zaidi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo milioni tatu.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha kuhusu fursa za mikopo ya TADB. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi (aliyesimama) akizungumzia changamoto zinazoikabilia sekta ya mifugo mkoani humo katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (wa pili kulia aliyesimama) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo ya mkoa wa Arusha. Kulia  ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.

Baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha waliohdhuria kikao cha pamoja na TADB wakitoa maoni yao kuhusiana hali ya hupatikanaji wa mikopo katika kusaidia sekta ya mifugo mkoani humo.
Ugeni kutoka TADB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wadau wa Mifugo mkoani Arusha mara baada ya katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO