Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwenyekiti wa Chadema Arusha Amani Golugwa akagua Uhai wa chama Longido

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Mhe.Amani Golugwa amefanya kikao cha ndani katika Jimbo la Longido Mkoani Arusha ambapo kikao hicho kiliudhuriwa na aliyekuwa Mbunge wa Longido Mhe.Onesmo Ole Nangole ,Viongozi, Kamati Tendaji pamoja na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Pia katibu huyo amewapokea wanachama wapya vijana kwa wazee waliojitokeza na kujiunga na CHADEMA na kuwapatia Kadi za uwanachama na bendera moja kwa kila mwanachama,amewaelekeza kuwa bendera izo ni kwaajili ya kutengeneza msingi katika sehemu wanayotoka.

Wanachama hao wapya walipokea maelekezo hayo kwa shauku kubwa na wameahidi wanaenda kulifanyia kazi swala hilo kwa weledi mkubwa kabisa,ili atakapo rudi Longido aje afungue misingi hiyo rasmi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO