Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kiwanda cha General Tyre mbioni kuanza uzalishaji

 

Sameer-Africa-TyreMfanyakazi akiwa kiwandani Sameer Africa Ltd, kiwanda kikubwa cha matairi nchini Kenya.

KIWANDA cha kutengeneza matairi na mipira ya ndani ya magari cha General Tyre, kinatarajiwa kuanza uzalishaji katika kipindi cha miezi 12 kuanzia sasa, imefahamika.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba aliwaambia wananchi waliotembelea banda la NDC katika maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzunguni mjini Dodoma.

“Uchunguzi wa kina, matengenezo na ukarabati wa mitambo na majengo, utaenda sambamba na unatarajia kukamilika Februari mwakani. Uzalishaji wa awamu ya kwanza utaanza baada ya kukamilisha mambo ya kisheria na Kampuni ya Continental AG, katika mwaka wa fedha 2012/13,” alisema Ngapemba.

Alisema maandalizi ya kukifufua kiwanda hicho yanatokana na uamuzi wa Serikali kuipa jukumu NDC, la kuhakikisha linatafuta mwenye uwezo na uzoefu katika biashara ya matairi.

Alisema shirika lake, limeshaanza kuwasiliana na wawekezaji walioonyesha nia ya kuwekeza katika kiwanda hicho kutoka China, Malaysia na Afrika Kusini, ambazo sasa zinakamilisha ukaguzi wa majengo na mitambo.

“Mkandarasi wa ukarabati wa majengo, anategemea kupatikana katikati ya mwezi huu na kukamilsha kazi mwishoni mwa mwaka huu,” alisema.

Kiwanda cha General Tyre East Africa Limited, kilianzishwa mwaka 1969 kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania, iliyokuwa inamiliki asilimia 74 ya hisa na Kiwanda cha matairi cha Marekani, General Tyre North America (CTNA), kilichokuwa kinamiliki asilimia 26.

Hata hivyo, mwaka 1987 CTNA iliuza hisa zake kwa kampuni moja ya Ujerumani. Kiwanda hicho kilishindwa kujiendesha mwaka 2007 na ilipofika mwaka 2009, kilifungwa.

Wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2012/13, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Abdallah Kigoda alisema, wizara yake kupitia NDC, inaendelea na mikakati ya kukifufua kiwanda hicho haraka iwezekanavyo.

PUBLISHED BY MTANZANIA JUMATATU, AGOSTI 06, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO