Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BULEMBO AUNGURUMA TABORA MJINI LEO, AZITAKA HALMASHAURI KUPELEKA FEDHA ZA MIKOPO KWA VIJANA NA KINAMAMA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.

 Pamoja na kuzungumzia taratibu za uchaguzi ndani ya unaoendelea katika ngazi za mashina, Bulembo amewataka wana CCM, kutambua kuwa sare za CCM zina thamani kubwa kwa kuwa ni za Chama tawala hivyo wazivae hata wanapokuwa wanakwenda kutafuta huduma katika maeneo muhimu, Amewataka pia madiwani kuhakikisha Halmashauri za wilaya zao zinatoa mgawo wa asilimia kumi fedha kutoka mapato yao, kwa ajili ya kuwapatika vijana na kina mama kwa ajili ya mikopo kwa kuwa utaratibu huo upo kisheria.
" Ndugu Bulembo Kazi hii ya Ukuu wa mkoa naipenda sana, hasa kwa sababu nasimamia ilani ya Chama changu, kwa niaba ya Wananchi wa mkoa huu, mpelekee Salaam, Mwenyetiki wetu, Rais Dk Magufuli, kwamba Tabora tunampongeza kwa kazi nzuri anazofanya, mwambie tuna imani naye na tutazidi kumuunga mkono", akisema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggry Mwanri alipotambulishwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wakionyesha bashasha na furaha kwenye kikao hicho
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggry Mwanri akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Mwalimu Queen Mwanshinga Mlozi, wakati wa mkutano huo
Mkuu huyo wa Wilaya ya Tabora mjini akisalimia kabla ya kuangusha kigeregere cha aina yake ambacho kilisababisha wajumbe kushangilia kwa uhodari wake
Kisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Tabora mjini akahakinikiza kigeregere chake kwa kupiga magiti 
Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuia ya Wazazi Makao Makuu, Ndugu Mgaya akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
Msaidizi wa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Ndugu Kalolo akisalimia baada ya kutambulishwa
Kishaa arindima kwa wimbo wa hamasa wa kabila la Wanyamwezi na baadaye kuporomosha mashairi yaliyosababishwa wajumbe kulipuka kumshangilia
Wajumbe wakiwa wamesimama wakati Mchungaji Elias Mbagatwa alipokuwa akitoa dua maalum ya kumuombea Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli Mungu amjalie kuendelea kuchapa kazi na afya njema, wakati wa kikao hicho
Mchuangaji Elias akiendelea na dua hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Ndugu Bulembo


Sheikh Hussein Mkamilwa wa Bakwata mkoani Tabora akiomba dua ya kubariki kikao kabla hakijaanza
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Mussa Ntmizi akifungua kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui Mussa Ntimizi akimkabidi Ndugu Bulembo zawadi ya asali
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Wakasubi akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya asali kwa Ndugu Bulembo
Kikao kikiwa kimefurika wajumbe, wakati Ndugu Bulembo akizungumza
Wajumbe wa kikao hicho akifuatilia kwa makini
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
Madiwani wa Tabora mjini wakishangilia 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
Ndugu Bulemo akisisitiza jambo
Madiwani wa Uyui wakisimama kuulizwa maswali na ndugu Bulembo
Mmoja wa wajumbe akifuatilia kwa makini kila kinachoendelea kwenye mkutano huo



Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akitoa ufafanuzi na kutoa maelekezo au maagizokuhusu maswali na kero zilizoulizwa na wajumbe kwenye kikao hicho, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO