Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA WAHUDHURIA KATIKA JUKWAA LA WAFANYABIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara mbalimbali wa nchini pamoja na Afrika ya Kusini wakati aliposhiriki pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika Jukwaa hilo  la Wafanyabiashara  jijini Dar es Salaam.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kutoka kwenye Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.



Sehemu ya Wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO