Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Meyawa Arusha na wenzake Waripoti Polisi na kutakiwa kurejea Ijumaa

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro pamoja na Viongozi wengine wameripoti kituo cha Polisi Arusha na kutakiwa kurudi tena Ijumaa wiki hii.

Meya huyo na viongozi wengine walikamatwa na kushikiliwa Polisi Kati Arusha kwa siku 2 kwa kosa la kupatikana katika kusanyiko bila kibali ambapo  walikuwa wanakabidhi rambirambi toka kwa wamiliki wa Shule Binafsi kwenda kwa wafiwa wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vincent.
Wengine waliokamatwa siku hiyo ni waandishi 10, Viongozi wa dini, walimu, mmiliki wa shule, madiwani na Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini. 
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO