Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA (TIRA)IMEZINDUA MFUMO WA KUHAKIKI BIMA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI


Kaishna wa Bima nchini Dkt.Boghayo Saqware akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog.


Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA)Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza akizugumza katika uzinduzi huo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu ya mkononi,uliofanyika Jijini Arusha leo,wa kwanza kulia ni Kamisha wa Bima Taifa Dkt.Boghayo Saqware,akifuatiwa na aliyepo kulia kwake ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman .Picha na Vero Ignatus Blog.
Meneja waTEHEMA kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Aron Mlaki akiwa anawonyesha namna ya kutambua Bima kama ni halali au ni feki kwa kutumia simu ya mkononi .Picha na Vero Ignatus Blog.
 Mkurugenzi wa masoko kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Bi.Adelaida Muganyizi  akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog

Baadhi ya washiriki mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo mfumo wa kuhakiki Bima kwa njia ya simu ya mkononi.Picha na Vero Ignatus Blog.
Afande James Manyama ambaye amemuwalikisha kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha akizugumza katika uzinduzi huo.Piha na Vero Ignatus Blog.

Mwanasheria wa Mamlaka ya usimamzi wa Bima (TIRA) Arthur  Mbena akiwa anawaelekeza wa kikosi cha usalama barabarani namna ya kutambua Bima kama ni halali au feki kupitia simu ya mkononi kwenye gari kama linavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus Blog.

 Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rwekiza (aliyevaa koti suti nyeusi)akiwa anamuelekeza dereva wa gari lililopo nyuma yao namna ya kutambua kama Bima iliyopo kwenye gari lake ni halali,ambapo gari Ehilo lilikuwa na Bima halali.Picha na Vero Ignatus Blog.
Elimu ikiendelea kutolewa namna ya kutabua Bima feki au halali kwa kutumia simu ya mkononi uliozinduliwa leo Jijini Arusha na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Picha na Vero Ignatus Blog.



Meneja wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Usiamizi wa Bima (TIRA)Aron Mlaki akitoa elimu kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani namna ya kutambua Bima feki au halali ,ni ya kampuni gani,Bima gari la matumizi gani,aina gani ya bima kubwa au ndogo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Igantus.Arusha

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini(TIRA)imezindua mfumo wa uhakiki wa Bima kwanjia ya simu za mkononi kanda ya Kaskazini ambapo zoezi hilo limeambatana na ukaguzi wa bima kwenye vyombo vya moto na kubaini bima feki katika baadhi ya magari na pikipiki.

Akizindua mfumo  huo kwa kanda ya kaskazini uliofanyika jijini Arusha Kamishna wa Bima Nchini Dkt.Boghayo Saqware amesema kuwa kampeni yao ina laengo la kuondoa bima feki sokoni ambazo  zinazouzwa ama kutengenezwa na wahalifu ,ambalo kwa mujibu wa sheria wanafanya kosa la jinai.

“Tumeanzia Pwani na sasa tupo Arusha na zoezi hili litakuwa endelevu,kwahiyo tunawaasa wananchi wanunue bima halali,tumezindua mfumo ambao ni rahisi kwa mtu anaenunua bima kujihakikishia kuwa bima hiyo ni feki au halali .”alisema Dkt.Boghayo.

Kamishna huyo amesema kuwa kwa miaka( 3) kesi (10) za Bima feki ziliamuliwa ,watu(5) walihukumiwa kifungo jela,(2) wamelipa  bilioni 20,000,000, hadi 40,000,000,mashauri ya jinai yaliyopo mahakamani yalifunguliwa mwaka 2016 Mbeya(1) Mafinga(2) Mara(1) na Dar es salaam (3) na kufikia jumla ya kesi mpya 7,ambapo mashauri yaliyopo kwenye uchunguzi wa polisi ni (10).

Kwa upande upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza amesema kuwa zoezi hilo katika Jiji la Arusha litaendelea kwa wiki nzima ambapo wataelekea Kilimanjaro ,Tanga ambapo amesema kuwa  10%  ya magari hapa nchini Tanzania hayana Bima halali,amesema hadi sasa hapa nchini kuna makampuni 31 ya Bima,mawakala 500 madalaliwa Bima ni zaidi ya 100.

“Kuna mtu akienda kukata Bima anakuwa hajui kuwa hiyo ni feki,na kuna mwingine aknajua kuwa hiyo ni feki na nashirikiana na yule anayemkatia,hivyo akibainika anafutiwa leseni mkatajia halafu taratibu nyingine za kisheria zinafuata kwani kwa utafiti ulikwisha kufanyika Jiji la Arusha ni la pili kwa kuongoza kwa pima feki huku Jiji la Dar es salaam kinara”alisema Rwekiza.I

Naye meneja wa Tehama Aron Mlaki (TIRA)ameelezea namna ambavyo mtu anaweza kuhakiki Bima kwa njia ya simu ya mkononi ambapo amezitaja njia kuu mbili ambazo ni inaweza kuwa kwa intaneti au njia ya ujumbe mfupi wa maneno.

“Kwa njia ya inteneti (una sechi mis.tira.go.tz ,utaletewa mahali pa kujaza ,hakiki stika kisha ukishahakiki stika inakuja ingiza namba za stika halafu bonyeza hakiki,utaletewa maelezo ya bima yako kama ni halali au feki,

 Kwa njia ya  ujumbe mfupi (unaandika  maneno stika unaweka namba ya bima kwa tarakimu zisizozidi 7 unatuma kwenye namba 15200 na hii ni kwa mitandao ya Vodacom na Tigo peke yake.”
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO