Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Meya wa Arusha Afunguka Maneno Mazito baada tu ya kuachiwa na Polisi leo


Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa  badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Aidha amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.
Meya, Lazaro aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.
Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha hizo kwa malengo mengine na kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa na kupeleka kwenye misiba ambayo ilitokea kipindi cha nyuma kama rambirambi.
Amesema wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga  jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.
“Yani hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si mimi bali nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa dini wafanye sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu nakamatwa kwa kosa gani ,na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo ambazo ni za rambirambi bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila Kata,”alisema na kuongeza;
"Mimi ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni.
 
"Moja ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri wa Kanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia.
"Maswali tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi wangu"
Naye  Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya hatafika mbali.
Awali jana Mei 19, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati akipokea msaada uliochangwa na wananchi kupitia tovuti ya  wezesha sasa ambapo alipokea msaada wa takriban shilingi milioni 4 alisisitiza kuwa wanasiasa waache kutumia msiba kwa kuingiza siasa kwani hakuna fedha yoyote ile iliyoliwa na pia wapo katika harakati za kuwatumia fedha wazazi pamoja na timu ya wataalam wa afya walioongozana na watoto wa Lucky Vicent ambao ni majeruhi wanaotibiwa nchini Marekani kama fedha za kujikimu na kiasi kilichobaki hadi sasa ni  zaidi ya Sh, milioni 56 ambazo kunakamati ndogo ya wazazi iliyoteuliwa ambao wataamua zitumikaje kwaajili ya kumbukumbu za watoto hao.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO