Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Ziara ya Mbunge wa Hai Katika Hospitali ya Wilaya ya Hai

Mbunge wa Jimbo la Hai, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi ya UpinzaniBungeni Mh Freeman Mbowe ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Hai kuwaona wagonjwa waliolazwa hospitalini na kufahamu changamoto mpya zinazoikabili hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo, Mhe.Mbowe ameongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Mhe. Helga Mchomvu pamoja na Katibu wa Mbunge huyo Irene Lema

Mhe.Mbowe alitembelea Maabara ya hospitali hiyo na kuahidi kusaidia maboresho ya mahabara hiyo kupitia mfuko wa Jimbo.

Aidha, mbali na kuzuru Hospitali ya Wilaya, Mhe.Mbowe ametembelea Shule za Sekondari katika Kata ya Machame Kaskazini, Masama Kusini na  Boma Ng'ombe.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai yupo Jimboni kwake kwa ziara mbali mbali kukagua maendeleo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO