Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SUMATRA YAKUTANA NA WADAU WA USAFIRISHAJI JIJINI ARUSHA KUKUSANYA MAONIYA KANUNI MPYA


Mkurugenzi na mdhibiti  Uchumi kutoka (Sumatra )Nahson Sigalla akizungumza na wadau wa usafirishaji katika mkutano uliofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa uchumi kutoka sumatra
Mwanasheria wa Sumatra  Judith Kakongwe akiwa anazungumza na wadau wa usafirishaji kutoka Mkoani Arusha na Kilimanjaro
Aliyeshika kalamu mkononi ni Afisa Mfawidhi Sumatra mkoa wa Arusha  Allen Mwanri, akisoma kabrasha alilonalo kwaajili ya kikao hicho .Picha na Vero Ignatus Blog.
Aliyepo katikati no mwenyekiti wa (RSA) Mkoani Arusha Bakari Msangi ,Aliyepo kulia kwake ni Katibu wa RSA Wilbard Gambeki  na wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa madereva wa Noa(NASA) Namanga.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wa kwanza kulia  ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waongoza Watalii Mkoani Arusha ndugu Halifa Msangi akifuatiwa na Katibu mkuu wa Chama hicho Immanuel Mollel .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wadau mbalimbali waluohudhuria kikao hicho kilichoandaliwa na mamlaka ya usimamizi wa usafirishaji ya nchi kavu na majini (Sumatra)
Wa kwanza kushoto ni ndugu mmiliki akiwananafuatilia kwa making yale yanayoendelea katika kikao hicho kilichoandaliwa na sumatara.
 Wadau wa usafirishaji na wamiliki wakiwa wanafuatilia yale yanayoendelea katika kikao hicho.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Wa kwanza kushoto ni muwakilishi wa Sumatra kutoka Mkoani Kilimanjaro akiwa na mwenyekiti wa kikao hicho ndugu ..
 Wa kwanza kulia aliyevaa koti jeusi ni Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani (RSA) Bakari Msangi akiwa anafuatilia kwanmakini yanayoendelea katika kikao hicho cha wadau wa usafirishaji na wamiliki kilichoandaliwa na Sumatra.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wa kwanza kulia ni Katibu mkuu wa chama cha wasafirishaji mkoa wa Arusha na Kilimanjaro Locken Massawe akiwa anapitia kabrasha katika kikao hicho.
Na.VeroIgnatus,Arusha.
Mamlaka ya Uthibiti wa vyombo Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA)hivi karibuni imefanya mkutano na wadauwa usafirishaji katika mkoa wa Arusha,lengo la kikao hicho ikiwa ni kupitiaRasimu ya kanuni zilizotengenezwa chiniya sheria ya leseni za usafirishaji,sura ya317,kanuni za usafiri wa magari naabiria ya mwaka (2017) Marekebisho yakanuni za leseni za usafirshaji wamagari ya mizigo(2017)na Marekebishoya Kanuni za leseni za usafirishaji wapikipiki (2017)
Mkurugenzi mdhibiti uchumi(SUMATRA) Nahson Sigalla amezitaja Rasimu hizo kuwa ni pamoja na rasimuya kanuni za leseni za usafirishajikwapikipiki, za magurudumu,rasimu yamagari yamizigo,amesema walichokiletakatika kikao hicho ni marekebisho yakanuni,ambapo amesema kanuni ileiliyokuwepo awali itaendelea kuwepo,bali walichokieta ni marekebisho
Amesema kuwa kwenye mabasi yaabiria amesema ni kanuni mpya ambayoitaiondoa kanuni ile iliyokuwepo hapoawali ya na kuiweka kanuni mpya yasasa ambapo wamewaita wadaumbalimbali ili waweze kupata maoni yao
‘’Tulichokileta toka awali kamailivyosema Rasimu tunategemea kupatamchango zaidi kutoa kwa wadau wamaoni ya namna ya kuboreha rasimu hiikama ambavyo wadau wanaendeleakuchangia hapa, kazi ya Sumatra katikakikao hiki ni kupokea maoni hayakuhakikisha tumeyaelewa baada yahapo tutakuwa nazoezi la kufanyaambalo tunahakikisha maoni ambayoyamepokelewa yanaingizwa katika hiikanuni.’’alisema Nasson.
Amesema kuwa mahali ambapo maoniyaliyotolewa yataonekana ni ya msingiyataingizwa kwenye rasimu ,amesemakuwa kikao kama hicho kimefanyikaArusha,Mbeya,Dar es salaam,naMwanza ,ambapo amesema kuwawadau waloshiriki kukao hicho wanayofursa adimu ya kuchangia mawazo yaokwa uhuru na uwazi ili kutoa mawazo yawale ambao hawajapata fursa yakukutana na mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Katibu mkuu wachama cha wasafirishaji mkoa waArusha na Kilimanjaro(AKIBOA) Lockenamesema kuwa katika Rasimu hiyoawali waliileta kwa lugha ya kingerezaikaenda kurekebishwa ikawa Kiswahiliwameirudisha vilevile ,amesemawanaiomba Sumatra watenganishemakosa ya na mwenye mmiliki nadereva ,kwani inaonekana kila kosawamelipeleka kwa mmiliki wa garijambo ambalo siyo sahihi .
“siyo kwamba tunaipinga kwa sababu yakudidimiza maswaa ya Sumatra hapana,ila kosa linalomuhusu dereva liwe ladereva ili aingie woga wa kufahamukuwa kosa lolote litakalo muhusu yeyendiyo atawajibika,lakini unapomuwekeammiliki wakati anayekuwa na gari mudawote dereva atapakia hata mizigohatarishi barabarani huku akijua kuwammiliki ndiye atahusika tunataka derevanaye abanwe.”alisema Locken.

Amesema kuwa faini iliyopo kwenyerasimu hiyo ni shilingi 250,000-300,000 kwa kosa moja au kifungo, amesemakuwa kutokana na hali ya uchumi yasasa kwao ni vigumu kuipata fedha hiyo,amesema wamewapa mawazo yao nawamewaomba wayapitiena aitengenezeupya na wawarudishie Rasimu hiyowaione wao kama wamiliki,ili waonekama inafaa kwenda Bungeni ndipowaibariki Waziri aipitishe.

‘’vinginevyo sisi kama wamilikiwasipofanya hivyo tutaikataa Rasimuhiyo, kwani faini iliyopo sasa hivi yaserikali kuu ya shilingi 30,000 hiyoyenyewe inatutoa jasho , hivi leoukiambiwa 250,000 au 300,000 si ndiyokwamba biashara unashindwa? sisitunatoa huduma jamani wamiki wotewamesinyaa kwasababu fedha hakunanauli hazipandi, vipuri vipo juu .’’alisemaLocken
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO