Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ajali ya pikipiki usiku wa leo, Moshono-Arusha

DSC01441

DSC01444 Kamera ya Blog hii ilinasa tukio hili la ajali ya pikipiki majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, katika eneo la Car-Wash, Moshono, nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Mwananchi huyu alianguka na pikipiki yake yeye mwenyewe na haijawezekana kujua kilichosababisha hali hiyo. Ilibidi Blog yako ijitolee usafiri ili kumuwahisha majeruhi huyu Hospitali ya Mt Meru ili kuokoa maisha yake mara baada ya kushughulikia PF3 kutoka kituo cha Polisi Kijenge Chini usiku huo. Majeruhi huyu alikuwa hajitambui na alikuwa akitokwa na damu mdomoni.

Alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba T580 BYR aina ya Toyo. Picha ya chini, waendesha bodaboda wakijaribu kutoa msaada wa haraka muda huo (Picha zote na Tumainiel Seria)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO